RC Gambo atoa onyo kwa watakaoandamana Arusha ‘Upanga haujaribiwi shingoni’
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ametoa onyo kali kwa watu watakaothubutu kuandamana mkoani humo baada ya kuzagaa kwa taarifa mitandaoni kuwa tarehe 26 April kutakuwa na maandamano ya nchi nzima.
RC Gambo amesema Arusha ni mji wa kitalii hivyo asingependa kuona usalama na amani inatoweka mkoani humo na kupoteza watalii ambao wanasaidia kukuza uchumi wa nchi.
“Arusha ni mkoa wa kitalii hatuwezi kuruhusu mambo yatakayoharibu uchumi na usalama wetu, kama kuna kikundi chochote kinampango kutujaribu, tunatoa tahadhari na kuwakumbusha kuwa upanga haujaribiwi shingoni,“ameeleza Mrisho Gambo kwenye taarifa yake.
Onyo la Gambo ni muendelezo wa maonyo mengine yaliyotolewa na viongozi wengine serikalini akiwemo Rais Magufuli juu ya watu watakaoandamana siku hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni