MASHINJI ASHINDWA KUFANYA MKUTANO ISAPULANO -MAKETE AKOSA WATU,HUKU MBUNGE VITI MAALUMU AKIISHIWA MAFUTA YA GARI NA KUSHINDWA KURUDI NJOMBE
Na Titho Stambuli
CHADEMA imezidi kukumbwa na Kimbunga cha CCM wilayani makete katika uchaguzi mdogo kata Isapulano, Pale ambapo mara kadhaa wamefeli kupata watu kwenye mikutano yao.
Leo Tarehe 09/08/2018 ,Katibu mkuu wa chama hicho amewasili wilayan makete kata ya Isapulano Vicent Mashinji akisindikizwa na mbunge viti maalumu kutoka mkoa wa Njombe Lucy Mlowe kupitia CHADEMA pamoja na Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mch.Peter Msigwa wamefika kwa ajili ya kuhutubia mkutano huo hali imekuwa ni mbaya pale ambapo wamekosa watu kabisa na kuamua kuahirisha mkutano maana wamejikuta wako watano.
Mkutano huo Licha ya kutangazwa lakini mwitikio wa watu umekuwa mdogo na kupoteza mvuto Kabisa, Hivyo viongoz hao wamelazimika kuahirisha mkutano huo na kuanza kuzurula wilayan makete huku wakikosa cha kufanya.
Mbunge wa Viti Maalumu Njombe Lucia Mlowe. |
CCM wameonekana kutembea kifua mbele na kuwasubiri jumapili wawalaze asubuhi na mapema
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni