Dstv Tanzania

KATIBU CCM -WILAYA YA MAKETE AONGOZA WAJUMBE KUTOA POLE ISAPULANO KWA WAATHIRIKA WA KIMBUNGA.

Katibu Wa CCM Wilaya ya Makete Cde-Langael Akyoo akiwa katika eneo la tukio.
CCM wilaya ya makete wamewafariji wananchi wa kitongoji cha Tunduma kata ya isapulano wilayan Makete.

Licha ya heka heka za kampeni za uchaguzi Kata ya isapulano lkn janga la asili limeikumba Kata ya isapulano 08/08/2018 majira ya usiku, kwa kimbunga kikali kuezua nyumba tatu Hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha, hivyo wananchi wengi wamekusanyika Kutoa Masada kwa waathirika wa janga hilo,
Vyama vya siasa vimelazimika kusimamisha shughuli na kufika kutoa Pole kwa waathirika hao ikiwa ni sehemu ya majukumu yake kusaidia jamii.

Akiongoza msafara huo katibu machachari anayetamba kuwalaza mapema asubuhi tarehe 12/08/2018,Cde-Langael Akyoo akiwa ameongozana na wajumbe wa kamati ya siasa mwkt Uvccm wilaya ya makete Nehemia Sanga, Joyce sigalla.

Katibu mwenezi wa wilaya hiyo yusuph sanga na katibu Uvccm wilaya ya makete na Kiongoz wa mkoa UVCCM mwenyekiti Nehemia Tweve.
Wamefika kwa walengwa hao na kutoa pole.

Akizungumza kwa niaba ya msafara huo katibu wa ccm wilaya ya makete.

"Ndugu zetu poleni sana na tatizo hili sote tumeguswa sana na janga hili Mwenyezi Mungu atupe Nguvu kwakuwa hakuna mwenye kuzuia majanga asilia, cha kushukuru hakuna aliyeumia, Ndugu zangu ccm tuko pamoja tunawapa pole na mpaka mwisho kuhakikisha ndugu zetu mnakuwa salama "
Wajumbe wote wametoa Pole .
Pia katibu ameahidi kutoa ushirikiano kwa kuishauri Serikali kutoa taarifa ya hali ya hewa wilayani Makete kuepuka majanga kama haya kwa wananchi ili waweze kuchukua tahadhari mapema.

Mtandao huu tunatoa Pole kwa waathirika Mwenyezi Mungu awape Nguvu ili muweze kurudi katika nyumba zenu.

Hakuna maoni: