Dstv Tanzania

MWANAMITINDO KUTOKA NJOMBE SAKINA EMMANUEL(Skyler) KUKULETEA ''USIKU WA KITENGE'' NI TAMASHA LA KUKATANA SHOKA



Na.Erasto Mgeni, Njombe.

Mwanamitindo kutoka Njombe Sakina Emmanuel maarufu kama Skyler Tar 25 /08/2018 anatarajia Kufanya  Tamasha la kukatana shoka linaloitwa  ‘’Usiku wa Kitenge’’

Akizungumza na StambulNews Sakina amesema siku hiyo ya tar 25 mwezi huu atakuwa na na usiku wa kitenge mkoani Njombe .ambapo ataonyesha mavazi aliodesign kwa kutumia kitenge.

Amesema Usiku huo watautumia kuonyesha asili ya makabila ya kusini namna  hapo kale walikuwa wanavaa mavazi gani.
Image may contain: Sakinah Emmanuel, standing
Aidha Amesema kuwa   na lengo la onyesho hili ni ,kurudusha asili na utamaduni wa mtanzania,vijana kutumia vipaji vyao kujiingizia kipato,vijana kuchangamkia fursa za rasilimali znazopatikana katika maeneo yanayotuzunguka.

Tayari kazi yake ya kubuni mavazi imeshaanza kuonekana kwani baadhi ya wananchi Mjini Njombe wameshaanza kutumia bidhaa anazozalisha kwa mikono yake.
 Image may contain: 2 people, people smiling, people standing, outdoor and nature
Kupitia Ukurasa wake wa Facebook  Sakina ameandika'' ni Usiku wa kitenge mkoani Njombe (kitenge night show) tar 25-8-2018 save the date place turbo hall karibun sana njoo tuonyeshe uzalendo na kufurahia kuzaliwa Tanzania kwa kutupia vazi la kitenge usiku huo yaan mwonekano asilia na mwanamitindo sakinah emmanuel pia nafasi za kudhamin onesho hili bado zipo thanks # Titho Stambuli# sakinah anakuambia thamini asili yako kuwa na muonekano asilia unaovutia please show love kwa kushare''
Umri wake wa miaka 21 unaonekana ni mdogo ukilinganisha na mipango mikubwa aliyonayo.
Image may contain: 1 person, smiling, standing and outdoor
Sakina anasema anatamani kuona ndoto yake ya kuifikia jamii kwa kiwango kikubwa inafakiwa.

Hakuna maoni: