Dstv Tanzania

BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA AMEMTEMBELEA ERASTO NGOLE (SHIKAMOOPARACHICHI) AMBAYE PIA NI KATIBU WA MWENEZI CCM MKOA WA NJOMBE KWENYE SHAMBA LAKE LA PARACHICHI.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania Inmi Patterson alipomtembelea katibu mwenezi mkoa wa Njombe Ndg Erasto Ngole  shambani kwake ambako analimia Parachichi.
Na.Titho Stambuli.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania amemtembelea katibu mwenezi mkoa wa Njombe Ndg Erasto Ngole nyumban na shambani kwake ambako analimia Parachichi zilizomtambulisha ulimwengu mzima na kumpa heshima kubwa kwa watu mbalimbali kwakuwa amekuwa akitoa elimu iliyowakomboa watanzania wengi.

Mwakilishi wa Serikali ya marekani amefurahishwa na kusifu jitihada za Kiongoz huyo kwakuwa na shamba la mfano la Parachichi.
Wa Kwanza Kutoka Kushoto ni Mke wa katibu mwenezi CCM Mkoa Njombe Erasto Ngole Ester Mwogofi Akiwa na Malozi wa Marekani Nchini Tanzania Pamoja na Maaofisa wengine.
Balozi wa marekani amemwambia Erasto Ngole kuwa Parachichi marekani linasoko kwakuwa linaboresha afya, linawaingizia kipato watanzania, na linatoa bidhaa mbalimbali ambazo zinatumika kama dawa ,Hivyo yeye kama balozi anawajibu wa kuona namna ambavyo wanaweza kuwasaidia wakulima hawa. 
Pia ameweza kujifunza namna ambavyo kilimo hicho wanafanya mpaka kufanikiwa kwa kilimo kikubwa namna hii, ameweza kuomba kujua changamoto zinazowakabili kwenye kilimo cha Parachichi kupitia kwa mratibu wa mtandao huo wa Parachichi mkoa wa Njombe.
Mh Erasto Ngole amemweleza balozi huyo kuwa changamoto kubwa inayowakumba wakulima hawa ni changamoto ya maji, na mbolea ambayo ndiyo huduma muhimu katika kuhakikisha wanavuna matunda mengi, lakini pia amemtoa wasiwasi mh balozi kuwa hali ya soko ni zuri la ndani na nje watu wengi wameinuka sana kutokana na kilimo hiki.
Mh Erasto Ngole amemuomba balozi huyo kuona namna ya kuweza kuwawezesha wakulima katika changamoto ya maji kwakuwa kwa sasa ndio mustakabali wa wananjombe wengi na limekuwa mkombozi wa kiuchumi.

Hakuna maoni: