WAZIRI MKUU: VIJANA FANYENI KAZI ACHENI KULALAMIKA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka vijana wabadilike na watafakari namna bora ya kuboresha maisha yao na wafanye kazi kwa bidii badala ya kukaa vijiweni na kulalamika.
Amesema
kama kuna changamoto zinawakabili katika utekelezaji wa shughuli zao,
basi watumie njia sahihi ikiwemo kuwasilina na viongozi husika waliopo
kwenye maeneo yao.
Aliyasema
hayo jana jioni (Jumatano, Agosti 8, 2018) wakati akizungumza na wakazi
wa kata ya Nandagala, wilayani Ruangwa katika mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye zahanati ya kijiji cha Nandagala.
Waziri
Mkuu ambaye ameambatana na mkewe Mary Majaliwa katika ziara yake ya
kikazi wilayani Ruangwa, alisema vijana wanatakiwa kujitambua na kuiunga
mkono Serikali kwa kufanyakazi kwa bidii.
Kadhalika,
Waziri Mkuu aliwataka vijana washirikiane kwa pamoja katika kubuni
shughuli mbalimbali zitakazowaingizia kipato, jambo ambalo litawakwamua
kiuchumi na kuwawezesha kujitegemea.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi hao mikakati mbalimbali
inayofanywa na Serikali katika kuboresha maendeleo ya wilaya hiyo
ikiwemo upatikanaji wa huduma za afya pamoja na maji safi na salama.
PiaWaziri
Mkuu aliwataka wananchi hao waendelee kuiunga mkono Serikali yao,
ambayo imedhamiria kuwatumikia ili waweze kupata maendeleo kwa manufaa
yao na Taifa kwa ujumla.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, AGOSTI 9, 2018.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni