Serikali yasema deni la Taifa ni himilivu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema hadi Desemba 2017, deni la Taifa lilikuwa limefikia Sh47.756 trilioni na tathmini zinaonyesha bado ni himilivu.
Akiwasilisha
mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ukomo wa
bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/19 mjini hapa leo Machi 13, 2018, Dk
Mpango amesema deni la nje lilikuwa Sh34.148 trilioni sawa na asilimia
71.5 na deni la ndani ni Sh13.607 trilioni sawa na asilimia 28.5.
Hata
hivyo amesema uwiano wa deni hilo na Pato la Taifa kwa mwaka wa fedha
2017/18 ni asilimia 34.4 ikilinganishwa na ukomo ambao ni asilimia 56.
“Uwiano
wa deni la nje na mauzo ya nje ni asilimia 81.1 ikilinganishwa na ukomo
wa asilimia 150. Hii inamaanisha kuwa uwezo wetu wa kulipa deni bado ni
imara,” amesema.
Amesema
Serikali inaendelea kuchukua tahadhari kwa kukopa kwenye vyanzo vyenye
masharti nafuu kuhakikisha mikopo hiyo inaelekezwa kwenye miradi ya
maendeleo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni