Dstv Tanzania

kilichofanya vikao vya bunge kukatizwa.


Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson leo asubuhi ameahirisha Bunge mpaka kesho saa tatu asubuhi kupisha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Buyungu Mwl. Kasuku Bilago aliyefariki siku ya Jumamosi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Akizungumza mbele ya wabunge wote waliokuwepo Bungeni siku ya leo Mei 28, 2018, Naibu Spika Dkt. Tulia amesema kuwa Wabunge watakao kwenda kuwakilisha kwenye mazishi hayo wataondoka Dodoma siku ya Jumanne asubuhi na kurejea Dodoma Jumatano mara baada ya mazishi hayo kumalizika.

"Kufuatia tukio hilo na kwa mujibu wa kanuni za Bunge siku ya leo hatutaendelea na kikao cha Bunge na badala yake tutakuwa na maombolezo ya msiba wa mwenzetu",amesema Dkt. Tulia.

Pamoja na hayo, Naibu Spika ameendelea kwa kusema "siku ya kesho tutakuwa na kikao cha Bunge kama kawaida isipokuwa tutahairisha Bunge saa sita mchana ili kutoa fursa kwa shughuli za heshima za mwisho kwa mwili wa marehumu Bilago na baada ya hapo tutaendelea na maombelezo hadi siku ya Jumatano".

Mwili wa marehemu Kasuku Bilango unatarajiwa kuzikwa Mei 31 nyumbani kwake huko Wilayani Kakonko, mkoani Kigoma.

Hakuna maoni: