Dstv Tanzania

MJUMBE WA KAMATI YA SIASA WILAYA YA NJOMBE ATEMBELEA KIWANDA CHA NJOMBE NATURAL FOODS CO. LTD. AHIMIZA WANANJOMBE KUPENDA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NYUMBANI.



MJUMBE WA KAMATI YA SIASA WILAYA YA NJOMBE ATEMBELEA KIWANDA CHA NJOMBE NATURAL FOODS CO. LTD. AHIMIZA WANANJOMBE KUPENDA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NYUMBANI.

Ndugu Jactan Mtewele ambaye ni mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Njombe, ametembelea kiwanda cha NJOMBE NATURAL FOODS. CO.LTD ,chenye maskani yake wilayan Njombe, kujionea shughuli ya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kama vile Njombe chill sauce, Juice, Tomato na Asali.

Mjumbe huyo ambaye amezidi kuchanua katika nyanja za siasa ameonekana kukidhi matakwa ya Tanzania ya viwanda, pale alipotembelea kiwanda cha kuzalisha bidhaa mbalimbali kwaajili ya matumizi majumbani, kuweza kujionea uzalishaji ,changamoto zake na kubadilishana mawazo kuona namna gan wanaweza kuongeza uzalishaji, viwanda vidogo vingine na vijana kutumia fursa kwa kushirikiana na SIDO wilayan Njombe.



Akifanya mazungumzo na mmiliki wa kiwanda hicho Bi mariet Putika, ameweza kumwelezea hatua za awali tangu anaanza kuzalisha bidhaa hizo alianzia nyumban kwa kuzalisha kiwango kidogo na baada ya kupata mitambo ameweza kuzalisha zaidi ya tani moja kwa siku na alifanikiwa kupata eneo la uzalisha katika kiwanda cha sido na baadaye sido kubadilisha matumizi ya eneo na hivyo kulazimika kurudisha mitambo ilipokuwa awali na kusababisha upungufu wa uzalishaji na baadhi ya wafanyakazi kupoteza ajira zao, Hivyo kiujumla wanachangamoto ya eneo la uzalishaji. 

Akimwelezea hali ya ushindani ya soko na yenyewe imekuwa ni tatizo kwa kuwa watu wengi wamekuwa wakipenda kutumia bidhaa kutoka nje ya nchi hali ambayo inachangia ugumu wa soko na kusababisha hasara kwa wakulima ambao wamekuwa wakiuza malighafi katika kiwanda hicho kama vile Nyanya, asali, pilili na matunda mengine, huku akisifu upatikanaji wa malighafi ni wa kiwango cha juu lakn soko linasababisha kupungua thamani kwa mazao hayo.



Ndugu mtewele akizungumza na mmiliki wa kiwanda hicho Ndugu Mariet Putika, amempongeza mama huyo kwa kuthubutu, kwani ameonyesha njia ya kutoa fursa kwa wengine kujifunza, ajira kwa watu, kuwahakikishia wakulima soko, kuchangia pato la taifa kuitangaza vyema Njombe na lishe kwa wanaNjombe. Ametoa wito kwa wadau mbalimbali mkoani Njombe kupenda kutumia bidhaa za nyumbani kwani kwa kufanya hivyo ni kuchangia kuinua viwanda vidogo vya nyumbani.




Naye meneja wa kiwanda hicho Ndugu Ndugu Francis Elia john ameshukuru ujio wa kiongozi huyo kwani wanapata faraja pale ambapo viongozi mbalimbali wanapo watembelea kwani wanapata muda wa kubadilishana mawazo namna ya kutatua changamoto mbalimbali na kuwaomba wadau kuzidi kuwatembelea na ameiomba serikali kupitia SIDO, kuwa karibu na wabunifu hao kwani wanaweza kukuza uchumi wa taifa na kuongeza ajira na amewaomba wadau wa Njombe kuunga jitihada hizo. 

Na mwisho Ndugu mtewele ameomba wadau wa Njombe kuweza kuunga mkono kiwanda hicho kwa kununua bidhaa hizo kwani kwa kufanya hivyo ni kuitangaza njombe kwa mema na kuongeza fursa kwa na kuwahakikishia soko wakulima wa nyanya, pilipili na matunda mengi,na kwa nafasi yake ameahidi kuzidi kushirikiana kwa karibu na kiwanda hicho na kutoa mchango wa kukitangaza na kutafuta masoko.


Kwa mawasiliano ya kiwanda

NJOMBE NATURAL FOOD CO. LTD.,
P. O. BOX 362,
TEL:0754745924
NJOMBE.

Hakuna maoni: