KUMEKUCHA DODOMA: BARAZA KUU LA VIJANA UVCCM TAIFA KUAMUA MAKUBWA LEO
Umoja
wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) unapenda kuufahamisha Umma wa
Tanzania na wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM na Vijana wote nchini
kwa ujumla, kwamba umepanga kufanya kikao chake cha kwanza cha Kikanuni
hapa Jijini Dodoma.
Kikao hiki cha kitafanyika leo Tarehe 31 Agosti,
2018. Kikao hiki kinafanyika baada ya kufanyika na kukamilika ka
mafanikio makubwa Mkutano Mkuu wa Tisa wa UVCCM ambao pamoja na mambo
mengine ulikamilisha safu ya Uongozi wa Jumuiya yetu pamoja na wajumbe
wa vikao vya Baraza Kuu Taifa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
Kikao
cha Baraza Kuu la UVCCM Taifa kilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya
Baraza Kuu la UVCCM Taifa na Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la
UVCCM Taifa vilivyovyokutana Jijini Dodoma jana Tarehe 30 Agosti, 2018.
Vikao vyote hivi vitaongozwa na Ndugu Kheri Denice James (MCC)
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa.
Vikao
hivi vinakaa kwa mujibu wa Kanuni ya UVCCM Toleo la mwaka 2017 ambapo
pamoja na mambo mengine vitakuwa na kazi ya kuchagua Wajumbe wa Kamati
ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa na kuwathibitisha Makatibu
wa Idara tano za UVCCM watakaopendekezwa kwa Baraza Kuu la UVCCM Taifa.
UVCCM
tunaamini kupatikana kwa wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji pamoja na
Makatibu wa Idara kutakamilisha safu yetu ya Uongozi na kutakuwa chachu
kwa Jumuiya kutekeleza majukumu yake ya Kikanuni na kwa mujibu wa Katiba
ya CCM kwa ufanisi mkubwa ili kukidhi matakwa ya Vijana wenzetu, Chama
na Taifa kwa ujumla.
Mwisho
tunawakaribisha wajumbe wote Jijini Dodoma kwa vikao hivi, kwani
maandalizi yote yamekalika na tunawatakia mafanikio na Baraka tele
katika vikao vyote vitakavyoanzia Tarehe 30 – 31 Agost, 2018.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Mwl. Raymond Stephen Mwangwala (MNEC)
KATIBU MKUU UVCCM TAIFA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni