MAKAMU MWENYEKITI CCM TANZANIA BARA AWASHUKURU WANANCHI WA KATA YA ITULAHUMBA -WANGING'OMBE,KWA MGOMBEA WA CCM KUPITA BILA KUPINGWA.
Makamu mwenyekiti
mzee Phillip Mangula ambaye yupo Nyanda za juu kusini kikazi ,ambapo
alifiika kata ya Isapulano kuhakikisha mpango kazi wa ushindi kata ya Isapulano
wilayani makete ,na kumnadi .
Leo 04 /2018
Msafara wa makamu Mwenyekiti umeambatana na viongoz kutoka
ngazi ya MKoa Mwenyekiti Jassery Mwamala,Katibu mkoa Hosea Mpagike , Mjumbe wa
kamati ya siasa mkoa Ngajilo ,Katibu wa wazazi mkoa Lucas Nyanda ,Mwenyekiti
UVCCM mkoa Nehemia Tweve na katibu uvccm mkoa Sure Mwasanguti.
Mangula amefika wilaya ya
wanging'ombe kuona hali ya kisiasa wilayani humo na mipango ya watendaji na
wanasiasa waccm kuhakikisha ccm inakuwa salama .
Lakini pia amefika kuwashukuru
wananchi wa kata ya Itulahumba ambapo kulitakiwa kufanyika uchaguzi mdogo wa
udiwani ,lakini ccm ilipitwa bila kupingwa ,Baada ya mgombea udiwani wa CHADEMA
kukosa sifa na Mgombea wa ACT kujitoa na kujiunga na ccm nakudai kuwa anaona
kazi nzuri inayofanywa na Raisi Dokta John Pombe magufuli ,hivyo hana sababu za
msingi za kupinga maendeleo anampisha mgombea wa ccm ili aweze kuharakisha
maendeleo ndani ya kata ya Itulahumba.
Umati mkubwa ulikusanyika makao makuu ya kata ya
itulahumba ukimsubiri makamu Mwenyekiti
, Mara baada ya kuwasili nyimbo na burudani zilitawala kabla ya kuingia
ukumbini.
Mh makamu Mwenyekiti amewahukutubia wananchi wa kata ya
Itulahumba Kwanza kabisa amewapongeza kwa umati uliofurika hii inaashiria kweli
ccm ni salama na anahakika itaendelea kuwa salama chini ya watendaji hodari .
Lakini pia amewashukuru wananchi hao kwa kukiunga mkono
chama cha mapinduzi kwa kuiacha ccm ipite bila kupingwa kwani inaashiria ccm
inakubalika na inafanya kazi kwa maslahi ya wananchi.
"Hiki ni kipimo tosha kuwa wanaitulahumba mnaimani na
ccm na mmeacha kuhangaika na vyama na mnataka maendeleo na chama chenye kuleta
maendeleo ni CCM"
Aidha Mh Mangula amewaambia wananchi wa Itulahumba kuwa
serikali iko busy na kuleta maji,umeme vijijini ,ujenzi wa miundombinu ,madawa
na ujenzi wa vituo vya Afya na elimu ,na kuhakikisha rasilimali za nchi hii
zinalindwa na zinamnufaisha kila mmoja .
Sisi hatuna ugomvi na wapinzani ila kwa sasa uwezo wa
kuongoza hawana na wakajipange nashukuru hata wananchi mnalitambua hilo wakomae
Kwanza hata kidemokrasia waive kisiasa ndani ya chama chao kwanza ndio waje
kuomba ridhaa ya kuongoza .
Zaidi Tazama Picha Hapa Chini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni