Dstv Tanzania

SIKUKUU YA WAKULIMA KITAIFA (nane nane) COMRED AWARD MPANDILA ASEMA ‘Wakulima,Wafugaji na Wavuvi’ NDIO TEGEMEO LA TAIFA KWENYE UCHUMI WA VIWANDA




SIKUKUU YA WAKULIMA KITAIFA (nane nane)

Anaandika COMRED AWARD MPANDILA

Siku ya leo ni siku ya wakulima "nane nane"

Kwa namna ya pekee napenda kuungana na wakulima wote nchini katika sherehe hii ya kitaifa.


Neno wakulima lina maana pana sana ndani ya mkulima kuna (wafugaji, wavuvi na mkulima mwenyewe) hawa wote kwa pamoja ndio tegemeo la Taifa kwenye uchumi wa viwanda wanabeba 75% ya uzalishaji mali


Katika kuelekea nchi yenye uchumi wa viwanda unaotekelezwa na serikali ya CCM chini ya Raisi wetu mpendwa Mh Dr. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI ambae kwa moyo wa dhati kabisa anahitaji kutufikisha kwenye uchumi wa kati basi kwa pamoja lazima tumuunge mkono kwa nguvu kwenye sekta hii ya wakulima ili kuzalisha malighafi kwa wingi tuweze kutoshereza viwanda vya ndani na kuunza nje ya nchi


TANZANIA YA VIWANDA NA UCHUMI IMARA INAWEZEKANA

KWA PAMOJA TUJENGE TAIFA💪🏼💪🏼💪🏼💪🏼💪🏼
Mtandao huu unawatakia kila la Kheri watanzania wote katika kusherehekea sikukuu ya wakulima na wafugaji .

Hakuna maoni: