WADAU WA MICHEZO MKOANI NJOMBE WAOMBWA KUICHANGIA TIMU YA MPIRA WA MIGUU YA WANAWAKE MAPINDUZI QUEENS FC
Na.Erasto
Mgeni,Njombe.
Wadau wa
Mpira wa Miguu Mkoani Njombe Wameombwa kuichangia Timu ya Mpira wa Miguu ya
wanawake inayofahamika kwa Jina la Mapinduzi Queens,michango itakayo wasaidia
Wachezaji wa Timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Soko la Wanawake Tanzania.
Wito Huo
Umetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa
Njombe Bi Rosemary Lwiva ambapo amewaomba Viongozi na wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi na Vyama Vingine vya Siasa Pamoja na Wadau wote wa Maendeleo Sekta ya Michezo Tanzania Kujitokeza Kwa Wingi Kuunga mkono
Mafanikio ya Timu Hiyo ambayo Msimu Uliopita ilifanya Vizuri Katika Soka.
“Ndugu viongozi na wanachama wa CCM na
vyama vyote wa mkoa wa Njombe tulikuwa na team ya mpira wa miguu ambayo
ilikuwa ligi kuu na sasa iko daraja la
kwanza naamini kwa umoja wetu itarudi tena ligi kuu maana inapeperusha bendera
ya mkoa wa Njombe” Amesema Bi Lwiva na Kuongeza “sasa mkoa wetu umebahatika
kuwa na timu ya wanawake inayotoka ludewa inaitwa Mapinduzi Queens ambayo tarehe
moja mwezi wa Tisa inaenda Tanga kwa
ajili soka la wanawake ni ligi kuu hivyo naomba tuwasaidie”
Mwenyekiti
Huyo wa UWT Mkoa wa Njombe Amesema kwa sasa Timu hiyo inahitaji msaada wa nauli,vifaa vya michezo na Chakula.
Hata Hivyo
Jukumu la Kukusanya Michango hiyo Kutoka kwa Wadau amepewa Balozi wa Shule za
Wazazi mkoa wa Njombe ambaye Pia ni Mmiliki wa Mtandao Huu wa Stambuli Media
Bwana Titho Stambuli huku akiwaomba wote watakao wiwa na kuinusuru Timu Hiyo
kuwasiliana na Balozi huyo.
“Balozi wetu
wa shule za jumuia za wazazi ndugu yetu Tito Stambuli anabeba jukumu hili la
kufanikisha hili naomba mawasiliano yote yapitie kwaTito Mtoto mdogo anayefanya
mambo makubwa Mungu awabariki sana nyote kwa mwitikio maana kwa pamoja tunaweza”Amesema
Bi Lwiva.
Kwa Upande wake Balozi wa Shule za
Wazazi mkoa wa Njombe ambaye Pia ni Mmiliki wa Mtandao Huu wa Stambuli Media
Bwana Titho Stambuli amesema Utaratibu wa namna Michango hiyo itakavyokusanywa utawekwe Muda Sio Mrefu na Kwa Yeyote ambaye atahitaji Taarifa zaidi awasiliane naye Kwa Namba 0754249545
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni