KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA KIZOTA DODOMA ZANOGESHWA NA MWL. MWANGWALA AKIMNADI DIWANI NGALYA(CCM)
Katibu
Mkuu Wa Umoja Wa Vijana wa chama cha Mapinduzi mwl Raymond Mwangwala
amemuombea Kura Mgombea Udiwani Kata ya kizota Ndg Jamali P Ngalya
katika Mkutano uliofanyika Mtaa wa kisabuje katika tawi la kisabuje
Wilaya ya Dodoma Mjini
Akimnadi
Mgombea huyo, Mwl Raymond amewataka Watanzania kujenga tabia ya
kuchagua viongozi watakaowasaidia na kuacha kuchagua ambao wakishapata
madaraka wanashughulikia shidao za matumbo yao badala ya shida za
wananchi waliowachagua.
Alisema
baadhi ya wa wananchi wamekuwa hawatazami sifa na uwezo wa mgombea
atakayewatumikia, badala yake kuchagua kwa kukurupuka kuchagua viongozi
ambao baadaye hawawasaidii kutatua kero zao, na hivyo kubaki
wanalalamikia serikali kuwa haiwahudumii.
#Tukutanekazini
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni