Dstv Tanzania

Picha: Lwandamina anena mazito baada ya kutua Botswana, Yanga SC yafikia hoteli ya Crystal Palace

Kocha mkuu wa mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga, Mzambia George Lwandamina, amesema kuwa mpinzani wake wa michuano ya klabu bingwa barani Afrika,Township Rollers FC wapo vizuri na wanacheza kitimu ila kwakuwa anafahamu soka la Botswana atahakikisha anachomoza na ushindi katika mchezo huo.

Yanga SC yakwea pipa kuwafuata Township Rollers ya Botswana
Lwandamina ameyasema hayo kupitia tovuti ya klabu ya Township Rollers FC mara baada ya kutua Gaborone nchini Botswana.
Rollers wanacheza kitimu, nafahamu soka la Botswana kwakua kaka yangu amecheza hapa. Timu niliiyona ikicheza katika ligi wa nacheza kwa ushirikiano.
Lakini tunamipango yetu wenyewe ya namna yakucheza kwa kuwa katika soka kilakitu ni mipango, kwa sasa tunaweza kusema tunazungumzia kipindi cha pili cha mchezo maana ni kama dakika 45 za kwanza zilishapita.

Hata hivyo Mzambia huyo hakusita kuzungumzia hali ya mazingira na urahisi wa usafiri ndani ya nchi hiyo.
Kuna urahisi wa usafiri hapa Botswana na hivyo mipango ya usafiri tumeifanya mapema.
Hatukuweza hata kufahamu kuwa miundombinu na vifaa vya kufanyia mazoezi ni vizuri hapa.
Yanga SC  ikiwa nchini Botswana itacheza mchezo wa marudiano dhidi ya Township Rollers FC  Machi 17  michuano ya klabu bingwa barani Afrika (CAF).

Hoteli waliyofikia Yanga SC nchini Botswana


Hakuna maoni: