Mamia wasafirishwa bure kwa treni kushuhudia uzinduzi wa reli
Shirika Hodhi la
Raslimali za Reli (Rahco) limetoa usafiri wa treni kwa ajili ya kuwapeleka
wakazi wa Dodoma katika eneo la uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa ambao
unafanywa na Rais Dk John Magufuli asubuhi hii Machi 14, 2018.
Mapema asubuhi,
wakazi hao wamekusanyika katika stesheni ya reli ya Dodoma kwa ajili ya
kusubiri usafiri huo, mabehewa sita yalikwenda mara mbili kuwapeleka watu eneo
unakofanyika uzinduzi huo katika stesheni ya Ihumwa mjini hapa.
Kufuatia usafiri huo,
idadi ya kubwa ya wananchi walijitokeza kushuhudia uzinduzi huo kutoka Morogoro
hadi Makutopora mkoani hapa.
Treni ya kwanza
iliondoka saa 1:20 asubuhi kuwapeleka watu eneo la Ihumwa na ya pili iliondoka
saa 2:46 asubuhi huku watu wengi wakiwa wamesimama.
Katika maeneo mengine
iliposimama treni hiyo kwa lengo la kuchukua watu wanaokwenda katika uzinduzi
huo, ilishindwa kuwachukua kutokana na kujaa kwa mabehewa hayo.
Hata hivyo, baadhi ya
abiria waliuokuwa na shauku ya kuutumia usafiri huo walikwenda na treni ya
kwanza na kurejea nayo tena mjini kabla ya kurudi tena Ihumwa kwa ajili ya
uzinduzi huo.
“Mimi sijawahi
kupanda treni hata siku moja, kumbe iko hivi nashukuru sana,” amesema Mwanaisha
Isasa mkazi wa Chang’ombe mjini Dodoma.
Uzinduzi huo
umehudhuriwa pia na wabunge na viongozi mbalimbali wa chama na Serikali.
Kaimu Mtendaji Mkuu
wa Rahco, Masanja Kadogosa amesema mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa kati ya
Morogoro na Dodoma ulisainiwa Septemba 29, mwaka jana kati ya Kampuni ya Rahco
na Yapi Merkezi Inssar Sanay’s ya Uturuki.
Treni hiyo ya
mwendokasi itakuwa ikisafiri umbali wa kilomita 160 kwa saa itajengwa kwa
gharama ya dola 3.457 za Marekani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni