Ofisi za mabasi ya mwendokasi zahamishwa
Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (Udart) umeamua kuhamisha ofisi zake kwa muda ili kuepusha uharibifu unaoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.
Ofisi
hizo zilizopo eneo la Jangwani, wilaya ya Ilala, kwa sasa hazitatumika
na mabasi yote yaendayo haraka yatalazwa katika vituo vikuu vya mabasi
hayo.
Akizungumza
leo Machi 16 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Udart, Deus Bugaywa
amesema wamehamisha ofisi hizo ili shughuli zinazofanywa na mradi huo
zisiweze kutetereka kutokana na mvua zinazoendelea.
"Maji
yalianza kujaa saa nane usiku, tulianza kuhamisha magari yetu yote na
kuyapeleka katika vituo vikubwa vya mabasi yetu, licha ya mabasi pia
tumehamisha vitu vingi vya ofisi kwa sasa hatutaitumia kwa muda,"
amesema Bugaywa.
Amesema
wameamua kusitisha huduma za usafiri wa mwendokasi leo, kutokana na
maji kujaa eneo la jangwani na hivyo barabara hiyo ilifungwua tangu saa
kumi alfajiri na imefunguliwa saa tatu asubuhi baada ya trafiki
kujiridhisha kwamba inafaa kupitika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni