Dstv Tanzania

KATIBU WA HAMASA NA CHIPUKIZI UVCCM MKOA WA NJOMBE NDUGU JOHNSON ELLY MGIMBA AWAGEUKIA WATUMISHI WA SERIKALI NA UVCCM WASIOSHUGHULIKA NA KERO ZA VIJANA -MAKAMBAKO.

Katika kuhakikisha anaungana na katibu wa Uvccm Wilaya ya Njombe -Daniel muhaza, Katika mapambano ya kuwatetea vijana wa Njombe,  kwa mara ya kwanza tangu kuchaguliwa kuongoza Kitengo hicho ameweza kuhudhuria kikao Cha Madereva Bajaji ambao waliwaomba kuja kuwasikiliza kero ambazo zinawakabili,ujio wa katibu wa hamasa katika mkutano huo ulifufua matumain ya vijana hao kuwa UVCCM ni jeshi imara la kutetea maslahi ya wanyonge, ambapo wamemueleza changamoto zinazowakabili na kutokupata majibu kutoka halmashauri husika ni pamoja na ubovu wa barabara waliyoamuriwa kupita, TRA washindwa kuwawekea mfumo rafiki wa ulipaji wa Mapato, Mzee Adam aliyewekwa na halmashauri ya mji kukamata bajaji zitakazo pita barabara Kuu na kutokuwepo na mtetezi wao katika ofisi zao.

Huku akina Dada nao wakimwambia Mgimba wengi tunapenda kazi Kuendesha bajaji lakini ubovu wa Barabara umekuwa kikwazo na wengi wamerudi Kufanya kazi wasioipenda ya kuuza Bar.

Licha Ya kuonekana kuduwaa na changamoto hizo zinazowakabili vijana na kusikitishwa namna ambavyo watendaji wa serikali wameshindwa kuwa wabunifu na kuwasaidia vijana .

Licha ya kuja kumuongezea nguvu Katibu wake akajikuta anawajibu wa kutafuta majibu ya vijana hao.

Kwanza kabisa amempongeza katibu wa Uvccm Wilaya ya Njombe Ndugu Daniel Muhaza kwa kutambua umuhimu wa kuwatetea vijana katika wilaya yake, amewasihi vijana hao kuwa watulivu Kwan hatakubaliana na hali hiyo ni lazima ataungana na katibu wa Uvccm Wilaya ya Njombe kuwafikia wahusika kwakuwa mkataba wao na CCM ni kuwatetea wanyonge iweje leo washindwe hayo?.

Ametoa mfano mfanyakazi wa duka lako akiwa hawezi kuwalinda wateja hafai atasababisha duka kukosa wateja na kufungwa, yupo tayar kuhakikisha mambo yanakaa sawa na kuhakikisha CCM inakuwa mstari wa mbele kuwatetea na watendaji wasio tufaa waondoke kwani wakati wa uchaguzi waoo wanafunga tai, CCM tunahangaika na kubanwa asema hatutarudia makosa tutanyooka nao mpaka kieleweke.

Katibu wa hamasa hakuishia hapo alionekana mwenye kiu kubwa ya kuonana na ma afisa vijana wa halmashauri hiyo lakini hakufanikiwa, alifika mpaka eneo la barabara ambazo bajaji zinapita na kujionea Hali halisi ilivyo na kukerwa na halihiyo na madereva hao wakimwambia wanalipa ushuru wa sh 500/= kila siku lakini ufumbuzi wa utengenezaji wa barabara hiyo mpaka leo Haujapatikan.

Pia amefurahishwa na Kituo cha polisi Makambako na kuwafagilia polisi Makambako Kwan wameonekana kuwa ni msaada Mkubwa kwa vijana hao, amewaomba kuendelea na moyo huo kwani ni nadra sana kuona makundi hayo yakishirikiana amefanya mazungumzo kwa kina na OCS wa kituo cha Makambako kuona ni namna gani Wataendelea kutoa msaada kwa makundi hayo.

Pia amempongeza katibu wa Uvccm Wilaya ya Njombe kwa juhudi zake ambazo ameonekana Kuzifanya kwa vitendo na kuomba watendaji wengine wa CCM hasa idara yake ya UVCCM kuwafikia vijana, kwani ili chama kizidi kung'ara ni lazima kuwatumikia vijana na wananchi kwa ujumla.

Imetolewa na Titho stambuli Mtokoma na Erasto K Kizumbe...... Kutoka ofisi ya siasa na uenezi mkoa wa Njombe.

Hakuna maoni: