MNEC NJOMBE APIGA HAT -TRICK WAPINZANI WAKOSA HOJA, APAKI BUS KUWASUBIRI 2019
Nguli huyo wa siasa mkoani Njombe MNEC -Fidelis lumato, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika shughuli ya kumsimika katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Ndugu Erasto Ngole, Tukio hilo kubwa na la aina yake lililofanyika Kata ya ramadhani kijiji cha itulike.
Nguli huyo ameonekana kutikisa tukio hilo kwa namna ambavyo hotuba yake iliyojaa mashiko na neema kwa wananchi wake na kusababisha wapinzani kukabidhi kadi na kufunga ofisi na kuhamia CCM muda huohuo wakati jambo hilo halikuwemo akilini mwao ni hotuba iliyosababisha wokovu huo.
Licha ya kila aina ya burudani na ushawishi wa Viongozi wa ccm, Hotuba yake ilionekana kama dawa ya Usingizi kwani utulivu ulikuwa wa aina yake na wapinzani kujisalimisha kwa wingi.
katika hotuba yake ameweza kugusa hali ya kisiasa, uchumi na amani.
Amewaomba wananchi kuwawatulivu kwani maendeleo hayawezi kuletwa na maandamano wala makerere ,wazidi kuwapa ushirikiano viongozi wa ccm na serikali kwani wamejipanga kuhakikisha wanatatua kero za wananchi na Kama kuna jambo linawasumbua wawasiliane na viongozi kwa karibu ili kuweza kulitafutia ufumbuzi, kwa kudhihirisha hilo aliweza kutumia vyema risala iliyosomwa na viongoz wa ccm kata ya ramadhani waliweza kuwasilisha kero za kata hiyo, haikuwa shida kwani tukio hilo lilihudhuliwa na viongozi wa serikali walioalikwa ilikuweza kujibu maswali ya wananchi waliokuwepo katika hafla hiyo na kuahidi kushughulikia kero zote kwa wakati.
Ameweza pia kuwaasa vijana kufanya maamuzi kwa maslahi ya taifa lao na sio kukurupuka na kupiga makerere wakati wamezungukwa na kila aina ya viongozi ni vyema wakafika kushauriana na hawana sababu ya kushinda wanahama vyama hali ambayo inasababisha wao wenyewe kujicheleweshea maendeleo.
Aidha amewaomba wanaccm kuwapokea Wale wote wanaorudi kutoka upinzani kwani wameokoka wawapokee na tuwasamehe kwa yote.
Namesisitiza umoja na mshikamano ndani ya CCM ili kuweza kuhakikisha asiye mwanaccm anaridhishwa na kujiunga na ccm ili kuweza kuharakisha maendeleo kwa wananchi.
Ametuma salamu kwa wapinzani wachache waliobaki na kuwaambia wasitegemee chochote uchaguzi ujao kwani kwa sasa hawana jipya na hawana hoja ya kuwaambia wananchi Kwani wananchi wameona wenyewe maendeleo ya kweli yanapatikana ccm ,hivyo waliobaki na wao wajitafakari.
na ofisi ya siasa na uenezi mkoa wa Njombe, Nguvu ya parachichi inahakikisha unahabarika
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni