ZIARA YA KATIBU WA SIASA NA UENEZI YALETA NEEMA MKOA WA NJOMBE.
Na Stambulititho, Njombe.
Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Njombe Ndg.Erasto Ngole Aprili 18, 2018 amefanya ziara wilaya ya Makete.
Ziara hiyo yenye lengo la kuimarisha uhai wa Chama Chama Mapinduzi na Kukangua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Ndg.Ngole alifika katika ujenzi wa jengo la Ofisi za Chama
Cha Mapinduzi wilayani hapo na kujionea ujenzi jinsi ulivyo kuwa
unaendelea na kuunga mkono ujenzi huo Ndg.Ngole alichangia sh 400,000/=
Ziara
hiyo iliendelea mpaka Kata ya Iwawa-Kijiji cha Ndulamo na kukagua
shughuli za ujenzi wa kituo cha afya ndulamo na kuongea na wananch na
kushirikiana nao kwenye kazi ndogo ndogo kwenye ujezi huo na kuchangia
sh 200,000/= kwa ajili ya kuwaunga mkono wananch wa kijiji hicho.
Pia Ndg.Ngole ametembelea Ofisi ya Mamlaka ya Maji Wilaya
Makete na kufahamu namna mamlaka hiyo inavyo wajibika katika Sekta ya
Maji na kupata maelezo ya Mradi
unao endelea kutekelezwa ili kupunguza tatizo la maji wilaya ya Makete,
Mradi huo unao tarajiwa kukamilika May 31,2018 kwa mujibu wa Meneja wa
Mamlaka huo.
Ndg.Ngole
alifika Kata ya Kipagalo Kijiji cha Madihani na kukagua Ujezi wa Ghala
la kuhifadhi Matunda na kuchangia sh.400,000/= na miche ya Parachichi
300.
Pia
Ndg.Njole alitimisha ziara yake Kata ya Ipelele ambapo alikagua ujenzi
wa kituo cha afya pia alichangia sh.300,000/= na miche 500 ya
Parachichi, huku akimzawadia Afisa tarafa sh.50,000/= kwa utendaji kazi
na kusimamia shughuli za maendeleo kwa umakini.
Wakati hakikamilisha Ziara hiyo Ndg.Ngole aliwapokea wanachama wapya wa Chama Cha Mapinduzi toka Chandema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni