KATIBU WA SIASA NA UENEZI MKOA WA NJOMBE AUNGANA NA WANANCHI WA KATA YA ITULAHUMBA -WANGING'OMBE KUMLILIA DIWANI TITHO MDENDEMI.
Na Titho Stambuli na Erasto kizumbe (NJOMBE).
"Wewe
ni Mungu utabaki kuwa Mungu, Hallelluya tutaonana mbinguni kwa Baba" Ni
nyimbo zilizotawala katika msiba Mkubwa uliotokea kwa wananchi wa kata
hiyo.
Ni
huzuni kubwa na pigo kubwa kwa wananchi wa Kata ya itulahumba na
wanaccm, Wilaya ya Wanging'ombe Mkoa wa Njombe, Baada ya kuondokewa na
Diwani wao kipenzi Titho Mdendemi aliyefariki na kuwaacha wananchi wake
wakibubujikwa na machozi wakiwa hawana la kufanya.
Katibu
Wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Ndg. Erasto Ngole amefika msibani
hapo akitokea ziaran makete ameungana na viongozi mbalimbali wa serikali
,dini, vyama vya siasa ,wanaccm nawananchi wa kata hiyo kuhakikisha
wanamuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele Diwani Huyo.
Katibu
Wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Ndugu Erasto Ngole amefika msibani
hapo akitokea ziaran makete ameungana na viongozi mbalimbali wa serikali
,dini, vyama vya siasa ,wanaccm nawananchi wa kata hiyo kuhakikisha
wanamuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele Diwani Huyo.
Akitoa
salamu kwa niaba ya ccm mkoa wa Njombe ametoa salamu za pole kwa
wananchi wa Kata hiyo na salamu za rambirambi, amewaomba wananchi
kumuombea na kuwa watulivu ccm inautaratibu wa kumpata kiongoz mwingine
anapotuacha watampata mrithi wake wa kiti cha udiwani,
Pia
amewakumbusha ndugu, jamaa na marafiki kuendelea kuwasaidia na kuwajali
watoto na mjane ambao marehemu amewaacha ,ili kuweza kuhakikisha ndoto
za watoto hao .
Ameweza
kumuelezea jinsi gani alivyomfahamu marehemu kwa uwezo Mkubwa alionao
wa kusimamia maendeleo ya wananchi wake, kujitolea, kujenga hoja na
kuhamasisha mshikamano ndani ya chama, na nje ya chama.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti wananchi wa Kata hiyo wamesema walimzoea kiongozi
wao na walimpenda Kwan alikuwa anawatumikia vyema wananchi wake hasa
swala la maendeleo na mshikamano ,wameumia sana lakini mwisho wa siku
sote njia yetu ni moja na kazi ya Mungu haina makosa -R. I. P titho
Mdendemi.
R. I. P -Diwani wa Kata ya itulahumba -wilaya ya Wanging'ombe (Titho Mdendemi)
MEMA YAKO YOTE TUTAYAENZI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni