Serikali ya Nigeria yatamani kufanya mazungumzo na Boko Haram
Serikali
ya Nigeria imesema ina mpango wa kutumia njia ya mazungumzo badala ya
kutumia nguvu za kijeshi ili kuwaokoa wasichana 110 waliotekwa katika
mji wa Daptch hivi karibuni pamoja na wale waliotekwa mjini Chibok mwaka
2014.
Ofisi ya Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari imesema ingependa kuwapata wasichana waliotekwa Chibok na Daptch wakiwa hai.
Utekaji
huo ndio mkubwa zaidi kufanywa na kundi la wanamgambo la Boko Haram
lenye itikadi kali ya Jihadi, tangu lilipowateka wasichana wa shule 270
katika mji wa chibok mwaka 2014.
Hata
hivyo, taarifa iliyowahi kutolewa na vyombo vya habari vya kiusalama
ilidai kuwa takribani wasichana 100 waliachiliwa huru na Boko Haram
baada ya kulipwa fidia na serikali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni