Twiga Stars yaingia kambini kujiandaa na AFCON
Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) imeingia kambini katika Hostel
za Makao Makuu ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT Mlalakuwa) kujiandaa na
mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake
AFCON 2018 nchini Ghana.
Kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars).
Twiga Stars itacheza dhidi ya Zambia (She Polopolo) Aprili 4, 2018 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na marudiano kufanyika April 8, 2018 jijini Lusaka nchini Zambia.
Mshindi wa jumla kwa raundi hii atacheza na mshindi kati ya Namibia v Zimbabwe mwezi Mei, na atakayeibuka mshindi atafuzu moja kwa moja kwa Fainali hizo za Wanawake Afrika.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni