VIONGOZI WA CCM MKOA WA NJOMBE WAMUUNGA MKONO WAZIRI WA TAMISEMI KUCHANGIA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI MAKOGA
Chama cha mapinduzi
mkoa wa Njombe kimeshiriki harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari
makoga ambapo mgeni rasmi katika harambee hiyo alikuwa waziri wa TAMISEMI MH
SULEIMAN JAFO.
katika harambee hiyo
viongozi kutoka ngazi ya Mkoa wamewakilishwa na viongozi wawili Katibu wa ccm
mkoa wa Njombe Ndugu Hosea mpagike na Katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe
Ndugu Erasto Ngole,Huku wilaya ya wanging'ombe ambao ni wenyeji wa shughuli
hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wa wilaya hiyo mzee kinyang'adzi.
Kwa pamoja wamejumuika na wananchi wa kata ya makoga na
wadau mbalimbali katika kuhakikisha ujenzi wa shule ya sekondari makoga
unakamilika kwa maslahi ya wananchi wa makoga na kwa matokeo chanya ya elimu.
CCM wameendelea
kudhihirisha kwa vitendo ilani ya uchaguzi pale kasi ya maendeleo inavyozidi
kupiga hatua n a wao kushiriki kazi na kuchangia maendeleo kwa maslahi ya taifa
letu.Na katika harambee hiyo ccm mkoa wameunga mkono kwa kuchangia mifuko ya
cement 100,Huku wilaya ya wangingombe ccm wakichangia shillingi
1000,000/=
.Harambee hyo
iliyokuwa na mvuto wa aina yake kwa wananchi kuhamasika kuchangia maendeleo na
kujitokeza kwa wingi na hata walioko mbali wameweza kutuma uwakilishi
,madhehebu nayo hayakuwa nyuma kuchangia huku CHADEMA wakitoa
shillingi 50000/=,kwa kutambua kuwa maendeleo hayana vyama.
Nao vijana wanaosoma
shule hiyo hawakuwa nyuma mchango wao wa burudani katika kuhakikisha
wanahamaisha wageni wao wanapata burudani ,Pia madiwani wa wanging'ombe na
watumishi kupitia umoja wao wameweza kuchangia Harambee hyo.
MH JAFO mwenye dhamana
na shughuli hiyo ameweza kukusanya shillingi million 137 ,Wanging'ombe
makusanyo mil 62 nayeye kupitia ofisi yake mil 75,Pia MH JAFO zawadi alizopewa
na wananchi wake ameweza kuomba vipelekwe kwa watoto yatima.
KWA PICHA ZAIDI ENDELEA KUTAZAMA CHINI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni