VIONGOZI WA CCM MKOA WA NJOMBE WAMUUNGA MKONO WAZIRI WA TAMISEMI KUCHANGIA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI MAKOGA
Chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe
kimeshiriki harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari makoga ambapo
mgeni rasmi katika harambee hiyo alikuwa waziri wa TAMISEMI MH SULEIMAN JAFO.
Katika harambee hiyo viongozi kutoka ngazi ya Mkoa wamewakilishwa na viongozi
wawili Katibu wa ccm mkoa wa Njombe Ndugu Hosea mpagike na Katibu wa siasa na
uenezi mkoa wa Njombe Ndugu Erasto Ngole,Huku wilaya ya wanging'ombe ambao ni
wenyeji wa shughuli hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wa wilaya hiyo mzee
kinyang'adzi.
Viongozi hao wamejumuika na wananchi wa kata ya makoga na wadau mbalimbali
katika kuhakikishaukarabati wa shule ya
sekondari makoga unakamilika kwa maslahi ya wananchi wa makoga na kwa matokeo
chanya ya elimu.
CCM wameendelea kudhihirisha kwa
vitendo ilani ya uchaguzi pale kasi ya maendeleo inavyozidi kupiga hatua n a
wao kushiriki kazi na kuchangia maendeleo kwa maslahi ya taifa letu.Na katika
harambee hiyo ccm mkoa wameunga mkono kwa kuchangia mifuko ya cement 100,Huku
wilaya ya wangingombe ccm wakichangia shillingi 1000,000/=
.Harambee hyo iliyokuwa na mvuto wa
aina yake kwa wananchi kuhamasika kuchangia maendeleo na kujitokeza kwa wingi
na hata walioko mbali wameweza kutuma uwakilishi ,madhehebu nayo hayakuwa nyuma
kuchangia huku CHADEMA wakitoa shillingi 50000/=,kwa kutambua kuwa
maendeleo hayana vyama.
Nao vijana wanaosoma shule hiyo
hawakuwa nyuma mchango wao wa burudani katika kuhakikisha wanahamaisha wageni
wao wanapata burudani ,Pia madiwani wa wanging'ombe na watumishi kupitia umoja
wao wameweza kuchangia Harambee hyo.
MH JAFO mwenye dhamana na shughuli
hiyo ameweza kukusanya shillingi million 137 ,Wanging'ombe makusanyo mil 62
nayeye kupitia ofisi yake mil 75,Pia MH JAFO zawadi alizopewa na wananchi wake
ameweza kuomba vipelekwe kwa watoto yatima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni