VIONGOZI WA UWT CCM-WILAYA YA NJOMBE WATOA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE KATA YA MJI MWEMA.
Mafunzo hayo yaliyoonekana kuwa na mvuto wa aina yake kwa wanawake kuitikia wito kwa kufika kwa wingi Huku jambo jema na la kupendeza pale wanawake kutoka CHADEMA walipojitokeza kwaajili ya kupata mema kutoka ccm.
Umahiri wa afisa mipango wa jumuiya hiyo Bi Grace Haule ambaye ni katibu mtendaji ameweza kuwaita watendaji wa serikali wenye idara hiyo ya maendeleo ya jamii kata ya mjimwema.
Ambapo lengo la semina hiyo ilikuwa ni kuwapa elimu wanawake hao ni jinsi gani wanaweza kuunda vikundi na kukopesheka na Halmashauri ya mji wa Njombe ,elimu ya ujasiriamali ambayo itawasaidia katika Biashara zao na uwezo wa kujitegemea kuwa na SACCOS yao ambayo itaweza kuwasaidia kujikopesha wao wenyewe.
Viongozi wa jumuiya hiyo kila mmoja kwa nafasi yake wameweza kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wanawake hao kwa umahiri na uwezo wa hali ya juu licha ya kuwa ni wabobezi wa siasa wameonekana kuwa na uwezo wa kuchangia matokeo chanya kwa jamii kwa namna ambavyo wanahangaika kuweza kumuinua mwanamke kwa namna moja au nyingine.
Licha ya kupewa semina hiyo wapo wanawake walionufaika moja kwa moja na zoezi hilo wale ambao walikuwa na kikundi lkn walikuwa wanashindwa namna ya kupata mkopo wakati wakiwa wamesajiliwa vizuri lakini namna ya kuwa na mawasiliano na Halmashauri.
Wanawake hao wameweza kupatiwa msaada wa namna ya kuweza kufanikiwa zoezi hilo kutoka kwa afisa maendeleo ya jamii na wengine wamenufaika kwa elimu hiyo na kuanzisha vikundi na SACCOS ambayo itakuwa inawanufaisha moja kwa moja.
Naye mwkt wa jumuiya hiyo Bi Angela Mwageni ameonyesha dira kuwa yeye pamoja na Katibu wake lengo lao ni kuja kuwa na SACCOS ya wanawake wilaya ya Njombe hivyo wanatia wito kwa serikali na wadau kuweza kuungana nao katika kuhakikisha wanafanikisha jambo hilo kwa maslahi ya jamii nzima.
Wakati mafunzo hayo yakiendelea katibu Mwenezi wa CCM aliwasili katika mafunzo hayo na kuweza kuwasalimia wanawake hao na kuwapa neno wanawake hao na kuwataka kuwa na umoja ili waweze kufanikiwa na kuwahimiza kufanya kazi ,yeye kwa nafasi yake atatoa ushirikiano wa kutosha na amewazawadia shillingi 500,000/= na miche 300 ya parachichi.
Amewataka kufanya kazi ili kujikwamua na umaskini na mwisho amewapongeza viongozi wa UWT kwa kuweza kuwatumikia wananchi hao kwa vitendo anawaomba wasikate tamaa kwani kumsaidia mwanamke ni kusaidia jamii nzima na pia ameahidi kuwezesha ziara ya mwkt wa UWT kata ya mjimwema Gari na mfuta kwaajili ya ziara yake katika kata yake
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni