DC HOMERA KUMALIZA TATIZO LA MAJI KATIKA VIJIJI MBALIMBALI WILAYANI TUNDURU.
Katika
kuhakikisha Wananchi wanapata huduma Muhimu kama Maji Safi na Salama, Mkuu wa
Wilaya ya Tunduru Juma Homera amewatembelea wananchi wa Vijiji vya Mkanyageni
na Mwongozo vyenye jumla ya Wakazi zaidi ya Elfu Kumi vilivyopo katika
Kata ya Mchuluka Wilayani humo wanaokabiliwa na tatizo kubwa la Maji baada ya
Visima vilivyokuwa vikitoa huduma ya Maji kupata hitilafu na kuwafanya
Wanannchi hao kukosa Maji.
Akiongea
na Wananchi hao katika nyakati tofauti wakati alipokwenda kuwajulia hali
sambamba na kupeleka Magari ya Maji safi aliyoyatoa kufuatia Ufadhili wa
AL-FILDAUS na Wadau wake,DC Homera amewataka wakaazi wa Vijiji hivyo kuwa
wavumilivu katika kipindi hiki cha Mpito kwani Serikali yao ya Wilaya tayari
imeshaanza Mchakato wa kuhakikisha Vijiji hivyo na vingine mbalimbali
vinapatiwa Maji safi na Salama.Aidha visima vinavyotarajiwa kuchimbwa ni 100
katika vijiji hivyo
Amesema
tayari wameshapa Mashine ya kuchimba Visima vya Maji vinavyotarajiwa kuanza
uchimbaji wa visima hivi karibuni chini ya ufadhili wa Taasisi ya
Kimarekani na mzawa Bwana Salim Kanyika HELP FOR UNDERSERVED COMMUNITIES (HUC)
Ameongeza
kuwa Visima hivyo vitakuwa Mwarobaini tosha wa kutibu na kumaliza tatizo la
Maji katika wilaya na Vijiji hivyo vilivyopo umbali wa kilometa Kumi na mbili
kutoka katika Mji wa Tunduru.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni