SADOCK MWANDA AFANYA KAZI YA MUNGU KWA VITENDO KATIKA KANISA LA PENTECOSTE HOLLINES ASSOCIATION MISSION TANZANIA, KATA YA HALUNGU -MBOZI.
Tumeagizwa
kujitolea na kumtumikia Mungu kwa muda ambao ametujalia afya na pumzi ya
kutosha hapa duniani .
Hayo
yamezidi kutimizwa na SADOCK MWANDA maarufu kama KADA KUTOKA SONGWE kwani Muda
mwingi ameonekana kutoa fadhila kwa makundi tofaututofauti,
Licha
kufadhili mashindano ya mpira wa miguu huko mbozi kata ya Halungu ,amemtumikia
tena Mwenyezi Mungu kwa kufanya kazi ya Mungu na nzuri yenye kupendeza pale
alipoongoza kuchangia Harambee aliyoalikwa kuwa mgeni rasmi katika kanisa la
PENTECOSTE HOLLINES ASSOCIATION MISSION TANZANIA,
Harambee
hiyo iliyokuwa na lengo la kuchangia ukarabati wa kanisa na ununuzi wa vifaa
vya muziki,ambapo katika Harambee hiyo ameweza kutoa kiasi cha shillingi
1000,000/=,kama mchango wake kuhakikisha kazi ya Bwana inaenezwa hapa Duniani
na yeye kama mkristo ameonekana kufanya vyema katika eneo la kumtumikia Mungu,
lakini pia
aliambatana na kada wa ccm kutoka Njombe Ndugu Titho stambuli ambaye aliweza
kununu CD moja kwa shillingi 500,00/=,Hakika Mungu akikubariki na akikupa ni
lazima ujitolee kwa wengine.
Hakika
kazi ya bwana ilifana na ilikuwa nzuri ,Bila kumsahau dereva wetu Erick melele
aliyetupeleka na kuturudisha salama.
Mashindano
ya mpira wa miguu yanaendelea chini ya udhamini wa Ndugu SADOCK MWANDA na
yatahitimishwa mwezi wa saba,Hakika wanambozi wanajivunia kuwa na mdau wa
maendeleo wa aina yake ambaye ameonekana kuwajibika vilivyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni