Dstv Tanzania

KATIBU WA HAMASA NA CHIPUKIZI UVCCM MKOA NJOMBE AIBUKIA NA KUSHEREKEA ID EL FITRI NA *VIJANA WA JUMUIYA YA WAISLAMU* CHUO CHA MGAO HEALTH TRAINING INSTITUTE.


Nguli wa siasa mkoan Njombe aliyejizolea umaarufu kwa kuwa kindakindaki wa ccm na mwenye viwango vya kimataifa ,Ndugu Johson Elly Mgimba ambaye ni katibu hamasa na chipukizi Mkoa wa Njombe,Ameibukia na kusherekea ID EL FITRI na vijana wa jumuiya ya waislamu chuo cha mgao health training institute ,kwani vyuo ni moja ya vijana ambao wako kwenye utawala wake hivyo analizimika kujumuika nao kuwaweka pamoja na kubadilishana mawazo.

Mgimba ameweza kutumia vyema siku hii ya sikukuu kwa kuweza kula chakula pamoja ,Kijana huyo mzawa wa Ludewa Nyota yake imezd kung'aa kila kukicha kutokana na uchapakazi wake ndani ya ccm na jumuiya yake na kuwa mchangiaji mzuri katika kujenga ccm yetu.

Ameonekana kuwa kimya kwa kipindi fulani kutokana na kubanwa na majukumu ya kikazi kwani anamiliki moja ya kampuni kubwa ya ujenzi Nyanda za Juu kusini na uagizaji wa magari.
Hivyo mda mwingi analazimika kuhakikisha kampuni zote zinakwenda ,huwezi kulisemea hilo ccm inaamn kiongozi ni lazima awe na kazi ni moja ya sifa ya kuwa kiongoz Hivyo ,Ndugu mgimba ameonekana kukidhi matakwa ya kiuongoz ndani ya ccm.

Wakizungumza kwa Nyakati tofauti viongoz wa chuo hicho wameonekana kufurahishwa na kiongoz huyo kwa kutenga muda wake na gharama zake kusherekea pamoja nao kwan wamepata muda mwingi wa kujifunza mambo mengi na kuchuma busara kutoka kwa kiongoz huyo.
Licha ya pongezi hizo wamemuomba kiongozi huyo kuendelea na kuwa na upendo wa namna hiyo kwani ni viongozi wachache wenye moyo kama wake hakika tumeridhishwa na kufurahishwa na kiongoz huyo mwenye sifa lukuki mkoan Njombe za kiuongozi.

Nyota huyo amebainisha kuwa uongozi kwake habahatishi ni karama yake hivyo anashukuru kwa kuaminiwa lkn pia anaomba watu wenye mapenzi mema na CCM wajenge mshikamano na kutenga mda wao kuweza kukutana na kukumbushana ahadi za ccm.

Mgimba Anaamin muda mwingi tunatumia kufanya kazi lkn ccm ndio chama kinachoongoza nchi hivyo ni lazima tutenge muda wa kutafakari ili kuweza kutoa mwelekeo sahihi wa taifa letu ,Aidha ameonekana kukemea makundi ndani ya ccm na kutaka utulivu kwani anaamn makundi hayajengi yanavunja umoja na kubomoa maendeleo yetu.
Na mwisho amepongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuwapa nafasi wanafunzi kushiriki siasa kwani viongozi huandaliwa na ameomba vyuo vingine kuiga mfano huo.

Hakuna maoni: