Dstv Tanzania

KATIBU UVCCM MKOA WA NJOMBE AWAAMBIA WANAZUONI KUTOKUCHAGUA KAZI ,WAJIKITE KATIKA UTAFITI WA FURSA NA KUONGEZA UBUNIFU.



Kiungo wa UVCCM mkoa wa Njombe ambaye ndiye mtendaji mkuu wa jumuiya hiyo katibu wa uvccm mkoa Ndugu Sure I Mwasanguti,kama kawaida yake kuandika kidogo matendo kibao,ameibukia kuwaasa wanazuon ambao wapo mtaani wakihangaika kutafuta ajira ambalo ni janga la Dunia kwa sasa.

Amewaomba vijana hao kuchangamkia kwanza fursa zinazowazunguka na kuwa wabunifu katika kuzitumia fursa kwani wkifanya hivyo wanawezajikwamua katika dimbwi la ugumu wa ajira na kujikwamua kimaisha na kusaidia jamii nzima na kutoa
ajira .

Akiwa kama mlezi wa vijana Mkoa wa Njombe ambapo kila kukicha amekuwa akiwajibika katika kuwapa mbinu mbadala vijana mbalimbali mjini humo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Lengo kuu ni kuwafungulia milango vijana ambao wamepata elimu lakini wanakumbana na changmoto ya ajira ,yeye kwa kutambua nafasi yake ya kuwatumikia vijana hayuko nyuma kila kukicha amekuwa nao begabega na kuwahamasisha kutumia elimu zao ili waweze kuwakomboa vijana wengine kwani wao kwa maono wametangulia ni lazima wawe wabunifu ya Darasani sasa wayahamishie huku mtaani ili na ambao hawajafika
Darasani waweze kuyafaidi mem Hayo.


Akisisitiza dhamira ya raisi wetu ni kuwaona watu wakifanya kazi na wawe wabunifu katika kuanzisha viwanda vidogo kwa kushirikiana na SIDO,serikali haitakuwa nyuma katika kussuport wabunifu kwani watasaidia kupunguza tatizo la ajira na kuchangia ukuaji wa pato la taifa.

Comrade mwasanguti amekuwa akitumia muda mwingi kukaa na wanazuoni ili kuweza kuwajenga kisaikolojia kwani wapo ambao wamekata tamaa,wakiamn katika kuajiliwa amewataka kutambua kunawasomi wengi kwa sasa hivyo mlango mkubwa wa ajira ni kujiajiri na ukibahatika kupata ajira ni jambo la kheri kwani ni lazima kila mmoja wetu alitumikie taifa pindi apatapo nafasi kwa
uwezo wake wote alionao na kwa kuaminiwa na taifa .

Huwezi beza kazi kubwa ya katibu huyu kwani tumeona kundi kubwa la wanazuon mkoan Njombe likionyesha mabadiliko chanya kwa wengi wao kujiajiri na wengine kuwa wajasiriamali wazuri walioanza kutoa huduma nzuri kwa jamii pale wanapoona kunafursa ,jambo jema kwa katibu huyo ni kuwapa maono vijana
walio mzunguka wanaanza kupata tabasamu kupitia maono yake.

Pia ametoa wito kwa wadau mbalimbali kuwasaidia vijana waliopo mkoani Njombe kwani wengi wanauwezo wa kufanya kazi kwani elimu wanazo na wapo ambao ni wabunifu wa hali juu hivyo yeye kama mlezi wa vijana kupitia ofisi yake atawajibika moja kwa moja katika kutoa dira kwa vijana na kuwalea hivyo anaomba wadau kujitokea kuongeza Nguvu.

Aidha katibu huyo ameenda mbali zaidi na kuwaambia wadau licha elimu walizo nazo wapo pia vijana wenye talanta tofauti mfano kucheza mpira ,muziki,mafundi na vipaji lukuki walivyo navyo ndani ya himaya yake hivyo anaomba wadau kujitokeza kuyaangalia makundi haya kwani wanaweza kujiajiri kupitia vipawa vyao na yeye kama mtendaji hatachoka kuwasemea na
kuwakumbusha wapi wanatakiwa kuelekea na kufanya nini.

Bado mengi usiyoyajua kutoka kwa mtendaji huyo mzawa wa ardhi yenye hadhi ya jiji- mbeya,amekuwa mstari wa mbele kuwahimiza vijana kuchapa kazi,anaupendo wa kugawa maarifa yenye matokeo chanya,uvumilivu wa hali ya juu hakuna asiyejua kazi kubwa ya kuongoza vijana karne ya leo , ni mlezi mzuri wa vijana na ni mpanaji haswa wa ccm kuhakikisha inaendelea kuwa
imara.

Aidha mtendaji huyo ameonekana kuridhishwa na kasi ya mwkt Ndugu Nehemia Tweve kwani amekuwa akimpa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha wanashirikiana katika kuwatuliza na kuwafunda vijana.Hivyo anakila sababu
ya kujivunia kuwa na mwkt mchapakazi.

Yapo mengi ya kukujuza juu ya katibu huyu nitaendelea kukujuza ....mema mengi ambayo anazidi kuyafanya ndani ya mkoa wa Njombe

Hakuna maoni: