BALOZI WA SHULE ZA WAZAZI CCM MKOA WA NJOMBE ASHIRIKI KAMPENI ZA UDIWANI WILAYAN MAKETE KATA YA ISAPULANO.
Cde-Titho Stambuli Mtokoma ambaye ni balozi shule za wazazi Mkoa Wa Njombe Masimbwe na Ludewa sekondari ameshiriki kampeni za uzinduzi wa Uchaguzi wa Udiwani wilayani Makete Kata ya Isapulano.
Balozi huyo ambaye ndiye
mmiliki Wa Mtandao wa stambulinews ameweza kutumia vyema ubalozi wake kwa kuwaambia
wanamakete hasa wa kata ya isapulano kujitafakari kwa kutokurudia makosa, kwani
ccm inadhamira ya kweli kuwaletea wananchi maendeleo.
Stambuli Ambaye ni kijana mwenye Uchungu na Maendeleo ya Taifa lake amesema wananachi wa kata hiyo awali walifanya makosa
ndio maana imewagharimu kwa kurudia Uchaguzi kwa sababu hata waliye mchagua ameshindwa
kuishi akiwa chadema na amerudi nyumbani.
''tumuunge mkono diwani huyu wanaisapulano ilituweze kupata maendeleo kwa haraka ni kumchagua Alphonce Mbilinyi. amesema Stambuli wakati wa ufunguzi wa kampeni hizo.
Amewahutubia wananchi hao kuwa wanatakiwa kuthamini na
kutambua kuwa serikali ya ccm inachapa kazi sasa kwa maslahi ya watanzania
wote, watu wa Makete serikali tayari imehaanza ukwenzi wa barabara ya lami,
shule, dawa mahospitalini na kupiga vita rushwa kuhakikisha wanyonge wanapata
haki.
"wanamakete msituangushe mtaweka kigingi cha nini kwa
kuwa hata mkiwachagua wapinzani wanarudi ccm hivyo tutakuwa tunapoteza muda na
kujicheleweshea maendeleo "
Yeye kama balozi mwenye dhamana ya kutangaza shule za wazazi
anawaomba wamchague ndugu Alphobce Mbilinyi kwakuwa atasaidia kusukuma
maendeleo ya isapulano na kuondokana na ubabaishaji na pia watakuwa wamethamini
na kuheshimu dhamira ya Raisi wetu kwa kumtengenezea chain nzuri ambayo
itasaidia kuwa na mtiririko mzuri wa kuleta maendeleo Isapulano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni