Dstv Tanzania

MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA MAKETE KUMPA ZAWADI RAISI DOKTA.MAGUFULI TAR:12/08/2018.

 Na Titho Stambuli.

Kiongoz Mkuu Wa CCM wilaya ya Makete Cde-Ona Nkwama ameonekana kutamba na Kutembea kifua mbele na mgombea wake wa udiw
ani kata ya Isapulano Ndugu Alphonce Mbilinyi.

Nkwama Amejigamba yeye na Katibu wake Langaelly Akyoo kuwa Mipango yote ya ushindi walishaiandaa na hivyo wanazidi kuchapa mwendo mpaka kieleweke arudi mshindi ndani ya ccm.

Mwenyekiti huyo ambaye ameonekana kuwa na mikakati na Mipango ya aina yake kuhakikisha anashinda bila shida yoyotee amezidi kutanua kuwa wapinzani mtauona moto wa ajabu pindi itakapofika tarehe ya uchaguzi.


Akiwahutubia wananchi wa kata ya Makete wakati wa mkutano wa ufunguzi wa kampeni amewaambia watu wa isapulano kuwa wameona muda walioupoteza kwa kuwa na kiongozi anayetokana na upinzani.

Ametamka kuwa yeye ndiye mwenye chama kinachoongoza serikali hivyo iliwaweze kupata maendeleo ni lazima mumchague diwani anayetokana na ccm ili awe na nguvu kwani hatapata kizuizi chochote wakat wa kutaka kufanikisha swala la maendele.

  "Wanaisapulano tangu mgombea wetu ajiunge ccm si mmeona shule ujenzi unakwenda,barabara na maendeleo yanamiminika ndani ya kata hii "


Hivyo ninawaomba wanaisapulano mnichagulie diwani anayetokana na ccm ambaye ni Alphonce Mbilinyi kwani yeye kama mwkt anapenda kuona isapulano inasonga mbele na kazi za maendeleo zinafanyika.

Pia amewaomba wanamakete kumpa shukrani ya Mh Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kumuongezea mtu ambaye atasaidiana naye katika kuleta maendeleo na kumshukuru kwa ujenzi wa barabara ya lami wilayani makete ujenzi Wa vituo vya Afya, shule na mikopo kwa wanawake na vijana, Hivyo amewaasa wanaisapulano kuhakikisha wanamchagua Diwani huyo. 


Yeye kama mwkt haoni sababu ya wananchi wa isapulano kurudia makosa na ametoa lai wananchi watakaokengeuka na pesa za wapinzani kwani hawatavumiliwa ccm tumejipanga na serikali imejipanga kuhakikisha wanadhibiti yote hayo atakayebainika hawatakuwa na huruma hatua zitachukuliwa bila kumuonea huruma. 


Ameongea kwa kilugha kuwa "wanamakete mliniamin mim kuwa mwkt wa ccm na leo naomba mniamini nawaambieni huyu ndiye Diwani atakayewafaa naomben mumchague "

Hakuna maoni: