CCM NJOMBE WAWASHA MOTO KATA YA ISAPULANO WILAYANI MAKETE, WAZINDUA KAMPENI KWA KISHINDO, WAPINZANI WAWEKA MPIRA KWAPAN MCHANA KWEUPE.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Njombe Jasery Mwamwala akiwa na Mgombea udiwani wa kata ya Isapulano Alphonce Mbilinyi wakati wa Uzinduzi wa Kampeni. |
Viongozi wa Chama cha mapinduzi (CCM)Mkoa Wa Njombe kwa kushirikiana na viongozi wa CCM wilaya ya Makete wamezindua kampeni Rasmi za uchaguzi wa Diwani kata ya Isapulano.
Unaweza kusema hii ni Ngumu kumeza ambayo imewakuta wapinzani pale kampeni hizo zilivyokuwa za nguvu na kwa kishindo huku wanachama wa vyama vya upinzani wamejiunga na ccm wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo na kuacha vyama hivyo vikipoteana.
Kushoto ni Katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe Sure Mwasanguti akiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Njombe Erasto Ngole. |
Mishare ya saa nane mchana moshi mweupe na wingu la kijani
lilitanda na nyimbo nzuri za ccm zikirindima huku wanachama wa ccm wakijimwaga
katika viwanja vya.
Baada ya mapokezi ya viongozi wa Mkoa na wilaya taratibu za
utambulisho zoezi zima la kuwahutubia wananchi lilianza ambapo viongozi
mbalimbali, walianza kuwahutubia wananchi kwa kuwaeleza wananchi mafanikio ya CCM , ndani ya kata hiyo, wilaya na watanzania kwa ujumla.
Mjumbe wa Kaamati ya Siasa mkoa wa Njombe Happyness Bomba Akimuombea Kura mgombea udiwani kata ya Isapulano |
Mwenyekiti Wa CCM Mkoa Wa
Njombe Ndg Jassery Mwamwala ameweza kuwaomba wanamakete kuweza kuchagua CCM kwa
kuwa CCM inadhamira ya kweli kuwakomboa wananchi wa kata ya isapulano.
Mwamwala amewataka
kutambua kuwa maendeleo ni mchakato na yanahitaji kuwa na chain nzuri raisi,
mbunge ,diwani na Mwenyekiti wa kijij ili kuwa na mlolongo mzuri.
''tusiweke kigingi na
tumtumie salamu vizuri mheshimiwa raisi na kumpa zawadi ya kumpa ushindi diwani
wa ccm ili kuweza kuleta maendeleo.''amesema Mwamwala.
Lucas Nyanda Katibu wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Njombe Akimuombea Kura Mgombea Udiwani. |
Wananchi kwa pamoja wameweza kuitikia kwa kiwango kikubwa
nakumuahidi kumpa kura za kishindo.
Sehemu ya Mamia ya Wananachi waliojitokeza katika ufunguzi wa Kampeni kata ya Isapilano |
Nao viongozi waliokuwepo katika uzinduzi huo wameweza
kusisitiza kuwa hakuna mbadala wa ccm na hakuna chama kingine chenye kuweza
kuwasaidia wanamakete zaidi hivyo wanatakiwa kumchagua Alphonce Mbilinyi ili
kuhakikisha maendeleo yanapatikana.
Mwenyekiti UWT Wilaya ya Njombe Angela Mwangeni akiburudika na wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa Kampeni. |
Viongozi waliohudhuria uzinduzi huo kutoka mkoan Njombe ni
Katibu Wa ccm Mkoa wa Njombe Hosea Mpagike, MNEC-Fidelis Lumato, Katibu Mwenezi
Erasto Ngole, Mwkt wa UWT wilaya ya Njombe Bi Angela Mwangeni, Katibu wa UWT
wilaya ya Njombe Bi Grace haule, Mwkt UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve na
katibu uvccm Mkoa Sure Ï Mwasanguti na Katibu Wa Jumuiya ya wazazi Ndugu Lucas
Nyanda.
Katibu wa Umoja wa wanawake wa CCM Wilaya ya Njombe Grace Haule akimuombea Kura Mgombea wa Udiwani. |
Viongozi hao wote kwa pamoja wameonekana kuweka mkazo kwa
wananchi kuweza kuhakikisha wanamchagua diwani huyo wa ccm ili kuweza kuhakikisha inapata maendeleo na inasonga
mbele kama kata nyingine zinazoongozwa na ccm, wampate Diwani anayeweza kubisha
hodi kila mahali bila kuulizwa na mtu na bila kupata kizuizi.
Viongozi hao kwa pamoja wamesema Diwani wa upinzan hana nafasi ya kuwasemea wananchi na hanauwezo wa kuwaongoza
wananchi kwa kuwa hana mnyororo wa kuweza kuleta maendeleo ya wanaisapulo.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Njombe Rosemary Lwiva naye hakuwa Nyuma kumuombea kura mgombea udiwani |
Akiwahutubia wananchi wa
isapulano Katibu wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpagike amewaambia wanamakete kuwa ''manaona ujenzi
wa shule, barabara, hospital zinajengwa zote hizi ni juhudi za ccm ndani
isapulano na sasa serikali ya ccm inahakikisha inafanikisha ujenzi wa barabara
ya lami makete to Njombe na Mbeya''
MNEC Fidelis Lumato akiomba kura |
Mpagike anawaomba wanamakete wampe zawadi
mheshimiwa raisi na wamshukuru kwa kazi nzuri anayoifanya kwa kumchaguliwa
diwani anayetokana na ccm ambaye ni bwana Alphonce Mbilinyi kwa kuwa
atatengeneza chain nzuri ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Isapulano.
Naye mgombea Wa udiwan kupitia tiketi ya ccm Alphonce
Mbilinyi ambaye mwanzo alitawala kupitia CHADEMA kuwa huko alikokuwa ni wasanii
watupu na anawaomba wamsamehe kwa kuwacheleweshea maendeleo kwani hakujua hivyo
amerudi Nyumbani kwani Nyumbani kumenoga.
Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve |
Amesena hakuna cha maana alichofanya
zaidi ya kuwapotezea muda na sasa ametubu anaomba wamchague ili aweze
kuwatumikia wanaisapulano na kuwaletea maendeleo wanaisapulano kwani anafahamu
shida walioipata pindi alipokuwa upinzani.
"Nasema hivi CHADEMA
Watapata tabu sana "
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni