CCM NJOMBE KUZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI KATA YA ISAPULANO WILAYANI MAKETE, Tarehe 29/07/2018.
Katibu wa Itikadi siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Njombe Erasto Ngole akiwa katika Kibao cha Shule ya Msingi Isapulano iliyopo Makete. |
Viongozi wa CCM mkoa wa Njombe kesho wataungana na wananchi wa kata ya Isapulano katika uzinduz wa kampeni za uchaguzi wa udiwani,viongozi Ngazi ya mkoa ambao wanasiku tano tangu wawasili wilayani humo,kushirikiana na viongozi wa wilaya kuendelea na maandalizi ya ufunguzi wa kampeni na kuwaomba kura wananchi kwa ujumla,ambapo maandalizi yameendelea kupamba moto ndani ya kata hyo.
Akizungumza na Stambulinews Katibu wa siasa na uenezi Mkoa wa Njombe Cde -Erasto Ngole amesema maandalizi yanaendelea vizur na hakika wamejipanga kufungua kampeni za uchaguzi wa Diwani.
Ngole Amesema CCM imejipanga vilivyo na imejiandaa kufanya vyema na wamejipanga kuwaeleza wananchi Wa kata ya Isapulano na wanamakete jinsi serikali ya CCM inavyofanya kazi kuhakikisha wanyonge wananufaika na rasilimali za taifa hili, kupiga vita rushwa na kuhakikisha maendeleo yanapatikana.
Amesema watawaambia wanamakete kuwa serikali imeshaanza kutengeneza Barbara ya lami,hivyo wasihangaike na vyama vya upinzani.
Watatua mkutano kuwaambia serikali ya ccm inavyozidi kuleta maendeleo ndani ya makete.
Wito kwa wananchi wa Makete wajitokeze kwa wingi katika ufunguzi Wa kampeni kesho waweze kusikia ccm inafanya nn kuliko kusikia habar za mitaan ya watu wasioeleweka.
''CCM na mgombea wetu tutakuwepo kumnadi mgombea wetu ili aweze kukamilisha mnyororo wa kuwaletea maendeleo wananchi na sio kuweka kigingi katikati''Amesema Ngole nakuongeza ''tunataka kuanzia raisi, mbunge, diwani mpaka mwenyekiti wa kijiji ili kuweza kuwapa na kuwasemea wananchi katika mtiririko uliosahihi''
Sime wanamakete Tukutane Isapulano
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni