VIGOGO CCM NJOMBE WAZIDI KUIKUMBATIA KATA YA ISAPULANO HUKO WILAYANI MAKETE.
Mji wa makete umezidi kuwatulivu, kutokana kishindo cha ujio wa vigogo wa ccm kutoka mkoani Njombe kuja kuungana na vigogo wa ccm Ngazi ya wilaya.
Leo mapema baada ya kugawana majukumu Kikosi maalumu kinachoongozwa na Katibu Mwenezi mkoa wa Njombe Ndugu Erasto Ngole chini ya usaidizi wa Comrade Mwasanguti katibu wa Vijana Mkoa Sure Ï Mwasanguti,Mwkt uvccm Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve na katibu hamasa wilaya ya Njombe Iman mahamoud moyo, wameweza kuzunguka kuhakikisha kata ya Isapulano iko Salama na tayari kwa maandalizi ya uzinduzi wa kampeni hapo kesho kwenye makao makuu ya kata hiyo.
Viongozi hao wameweza kuhakikisha wanachama wa CCM na wapya waliojiunga wanakuwa salama.
Hakika Naweza kusema mambo yaliopo Isapulano ni zaidi ya kutafuta ubunge CCM imedhamiria kushinda kwa asilimia kubwa kwa jinsi maandalizi yalivyo na vigogo hao wamepanga kuwepo wilayani humo ndani ya kata hiyo mpaka uchaguzi unaisha.
Zaidi tazama hapa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni