CCM NJOMBE WATUA MAKETE-KATA YA ISAPULANO TAYAR KWA MASHAMBULIZI YA UCHAGUZI,WAAPA KUIRUDISHA KATIKA HIMAYA YAKE.
Viongozi wa CCM na makada
kutoka mkoa wa Njombe wametua wilayani
Makete, tayari kuwapa homa ya uchaguzi wapinzani ,Timu hiyo ya ushindi
imeongozwa na Katibu Wa mkoa Wa Njombe -Hosea Mpagike akiambatana na safu yake
Katibu Mwenezi mkoa Wa Njombe Erasto Ngole, Katibu Wa wazazi Mkoa Lucas Nyanda.
Kushoto Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Njombe Nehemia Tweve,Katibu UVCCM Mkoa wa Njombe Sure Mwasanguti na Imani Moyo Katibu wa Hamasa na Chipukizi wilaya ya Njombe. |
Ilikuwa ni mshangao kwa wenyeji kuona msururu wa magari ukiingia wilayani Makete na bendera za ccm zikipeperushwa, huku makada wa Chama hicho wakipga vigeregere na nderemo wakiashikilia nguvu ya mashambulizi imeongezeka na wanauhakika kata hyo itarud ndani ya CCM.
Baada ya kuonana na wenyeji wao mwkt na Katibu Wa wilaya hyo
Akyoo walijifungia na kufanya kikao kizito kwa muda wa masaa matatu, Baada ya
kumaliza kikao walitoka kijeshi magar yote yalitawanyika kuelekea kata ya
isapulano ambapo kila gari likielekea kwenye kijiji chake kadri walivyopangana
kufanya mashambulizi.
Simanzi kwa wapinzan kwani walikuwa kwa mguu huku wakiwa
wameduwaa hawana la kufanya na bendera zao, na wengine kutimkia ccm na wachache
kubakia mayatima na huzuni ,huku wanachama Wa ccm wakiangua kicheko ishara ya
ushindi na wameapa ushindi wa nguvu kwani wamechoka kucheleweshewa maendeleo.
Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM Mkoa wa Njombe Erasto Ngole Kushoto akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Njombe Comred Nehemia Tweve wakiwa tayari kwa Kazi. |
Huku katibu Mwenezi amekutana uso kwa uso na aliyekuwa mgonbea
wa ACT halafu akarudi CCM, amemuomba radhi kiongozi huyo huku akidai yupo tayar
kuhakikisha ccm inashinda na amewaomba wanachama aliokuwa nao huko kurudi kwani
wamepotea hakuna mbadala wa ccm kwenye kuwaletea maendeleo wananchi.
Hivyo haoni sababu ya yeye kuwa huko anawaomba waje
wajumuike na chama chenye demokrasia ya kweli na kuwataka wananchi kutambua
dhamira ya kweli ya mheshimiwa raisi, akitolea mfano wa barabara inayochimbwa
tayar kwa kutengenezwa kwa kiwango cha lami hivyo haoni wanamakete kuanza kukengeuka.
Wananchi tofauti tofauti wakiongea na stambuli news
wameonekana kuridhishwa na serikali ya ccm inayoongozwa na Mh raisi wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dr John pombe
Magufuri, ilivyojikita kuwasaidia wanyonge na kuwaletea maendeleo watanzania
,hivyo wengi wamekuwa na imani na ccm na sasa chama kimekuwa cha wanachama
hivyo vyama vingine vinapoteza muda tuu.
Zaidi Tazama Picha hapa Chini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni