Dstv Tanzania

MJUMBE HALMASHAURI KUU CCM MKOA WA NJOMBE AWAAMBIA WAPINZANI CCM HATUTAVUMILIA KAMPENI ZA VURUGU


Na stambuli titho .

Mjumbe wa halmashauri kuu ccm mkoa wa Njombe Ndugu Vasco Mgimba ,kutoka wilayani Ludewa kata ya Ludende amepinga vikali kampeni za fujo na matusi ambazo Zimekuwa zikifanywa na Vyama vya Upinzani  wakati wa kampeni..

Mgimba amaesema Wao kama Chama wamejipanga kufanya kampeni za ustaarabu Lakini endapo watafanya vurugu vyombo vya dola vitawashughulikia kwa yeyote atakaye vunja sheria awe CCM ama upinzani.

"Tunawachelewesha wananchi kufanya maendeleo kila mtu ajinadi na aendelee kuchapa kazi". amesema Mgimba na Kuongeza ''Tumechoka kampeni zao za vurugu kila siku matamko yasiyo na tija kwenye vyombo vya habari.


Kadhalika amesema CCM ni chama kikubwa hakitakuwa na muda wa kupoteza katika hilihuku akiwataka kuacha kuhangaika kwani wananachi  wanaelewa serikali ya CCM  inavyowajali wanyonge na kwa maslahi ya taifa hili.

''kimsingi sioni kama ccm itashindwa uchaguzi asubuhi na mapema kweupe tunabeba kata zote pia amewaomba madiwani walioko upinzani watimke tuu waje ccm wachape kazi.''
  

Hakuna maoni: