Dstv Tanzania

NJOMBE KUSINI YAMDUWAZA MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM (M) NJOMBE.


Mwenyekiti  wa wazazi CCM  mkoa wa Njombe Ndugu Josephat Mpogoro  ,ameendelea kuchanja mbuga na ziara jimbo la Njombe kusini na msafara wake, aliombatana nao katibu wa wazazi mkoa wa Njombe Ndugu Lucas Nyanda ,na wenyeji wao wakiongozwa na Mwkt wake kasanga makweta na katibu wake Ndugu Ngogo ,Mwenyekiti  amefanya ziara Jimbo la Njombe Kusini ambalo linatawaliwa na mbunge Edward Mwalongo.

Mwenyekiti ameweza kuzifikia Kata za Iwungilo na Uwemba ,ziara hiyo iliyobeba jumbe mbalimbali kama vile kushukuru kwa kumchagua, elimu ,malezi ,uchumi,na uimarishaji wa Jumuiya hyo .


Baada ya kuwasili katika jimbo hilo mwkt amepokea report ya kiutendaji ndani ya kata hizo mbili ambapo wamemweleza mwkt jumuiya iko salama na chama pia ,ushirikiano mzuri na serikali na jumuiya nyingine na wanaendelea kuhakikisha jumuiya iko salama wao kama wazazi kwani wanatambua jukumu lao la kwanza ni  kuhakikisha jamii inakuwa salama hasa upande wa elimu , malezi,uchumi na Afya.


Lakini  pia wamemweleza mwenyekiti  mafanikio yote hayo changamoto bado ni nyingi zinazoikabili jumuiya hyo kata ya Iwungilo wamesema ikiwamo kutawaliwa na upinzani hili linaleta kutokuwa na mwakilishi anayeweza kuwasikiliza wao kama jumuiya ya wazazi na kutengeneza muunganiko mzuri.
Baada ya kupokea risala hiyo Mwkt ameweza kuwahutubia wanachama wa jumuiya hiyo kwanza ameanza kuwapongeza kwa kumchangua kuwa mwkt wa mkoa wa Njombe,lakini amewapongeza wazazi kwa jitihada wanazozifanya katika swala zima la Elimu ,Malezi na Uchumi kwani anaona jitihada mbalimbali mnazozifanya za serikali huku akisisitiza zaidi swala la elimu kuwapeleka watoto shule na kuhakikisha wanapinga vikali mimba za wanafunzi kwani zimekuwa zikiathiri maendeleo ya elimu kwa mtoto wa kike.

Pia amewataka wazazi kusimamia kidete swala zima la malezi kwani jamii ya sasa imezidi kupotoka na kuharibika kimaadili jambo ambalo linaathiri maendeleo ya Jamii ,mwkt amesema taifa lolote lile bila maadili mazuri katika jamii haliwezi kuendelea hivyo amewataka wazazi kuwalea watoto katika maadili mema .

Lakini pia amewaasa wazazi hao katika swala zima la kutunza Mali na kuhakikisha wanakuwa na uchumi unakidhi matakwa ya kuwafanya wapate huduma kwa wakati,ameonekana kukemea umaskini uliokithiri ,amewataka kutumia vyema rasilimali zinazowazunguka ili kuweza kujikwamua katika janga la umaskini .


"Usipokuwa na hela utakufa mapema ", amefafanua utakosa chakula ,matibabu na utashindwa kuijengea uwezo familia yako .


Naye katibu wake Ndugu Lucas Nyanda ameonekana kumuunga mkono mwkt kwa kukubaliana na hotuba yake kwa kuhakikisha wazazi wanahakikisha jamii inakuwa salama,kwani wanawajibu wa kuhakikisha wanasimamia vizur maswala ya elimu,mazingira ,Afya,na uchumi kwani wakisimamia yote haya jamii inakuwa salama na hawatayumbishwa na mtu yeyote na kuacha kutapatapa.


Mwenyekiti ameweza kuwaomba wanachama wa kata zote hizo mbili kuendelea kuwa na mshikamano na umoja ili kuweza kusaidia kujenga taifa hili ,ametolea maelezo changamoto ndogondogo zinazowakabili wanachama hao yeye pamoja na ofisi yake amezibeba na atatoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha wote tunakuwa salama na ccm inazidi kuwa imara na mshikamano na kuendelea kushika dola.


Zaidi Tazama Picha hapa Chini.


Hakuna maoni: