CCM kufuatilia mijadala ya wanachama wake mitandaoni
Dodoma. Katibu Mkuu
wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema chama hicho kinafuatilia majadiliano ya
wanachama wao katika mitandao ya kijamii ili kujiridhisha kuwa haivuki mipaka
ya uhuru wao.
Akizungumza leo
Ijumaa Agosti 31, 2018 katika ufunguzi wa baraza kuu la vijana wa chama hicho
(UVCCM) amesema mitandao hiyo imekuwa chanzo cha fitna, kebehi na kuchafuana.
Amesema wakati
mwingine mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli anachafuliwa katika mitandao
hiyo na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa na UVCCM kulinda hadhi ya taasisi ya
urais na chama.
“Tunafuatilia
mijadala ya wanachama wetu wote ndani ya chama na jumuia ili tujiridhishe
hawavuki mipaka ya uhuru wa kujadili masuala ya chama ndani ya mitandao hiyo,”
amesema.
Ametoa mfano wa
kiongozi mmoja (bila kumtaja jina) wa UVCCM mkoani Mara kuwa alikuwa
akiingilia masuala ya kisheria na kuandika mambo ya ovyo mitandaoni kuhusu
Serikali.
Amesema mambo
aliyokuwa akiandika kiongozi huyo hayakuwa na ukweli na hivyo kusababisha
taharuki.
“Pamoja na ujana wenu
katiba zetu na kanuni hazina eneo ambalo limeandikwa mikutano na vikao katika
mitandao ya jamii. Mnapoteza muda na kujidhalilisha kuanza kujadili mambo
ambayo yalitakiwa kujadiliwa kwenye vikao,” amesema.
Amesema wanawategemea
vijana kutangaza mambo ya chama lakini wanayotakiwa kuyatangaza ni yale
yaliyokwishajadiliwa katika vikao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni