SASA NI MWENDO WA TOT NA VIJANA JAZZ,CHAMA CHA MAPINDUZI SASA KUTUMIA BENDI ZAO TU.
Dodoma. Katibu Mkuu
wa CCM Dk Bashiru Ally amesema chama hicho hakitakuwa na bajeti kwa ajili ya
wasanii na badala yake watabaki na vikundi vilivyopo ndani ya chama.
Ametoa kauli hiyo leo
Ijumaa Agosti 31, 2018 wakati akifungua mkutano wa baraza kuu la Umoja wa
Vijana wa chama hicho (UVCCM) jijini Dodoma.
Alipotafutwa na kutoa
ufafanuzi kuhusu kauli yake hiyo, Dk Bashiru amesema kwa sasa wasanii
watakaoshiriki shughuli za chama hicho, watapewa huduma muhimu pekee ikiwemo
malazi, chakula na usafiri.
Akifungua mkutano
huo, amesema msanii wa Afrika ni mwana mapinduzi, mpambanaji na kwamba mashairi
ya wimbo wake ni lazima yawe na hisia zinazowakera na kuwazomea wanyonyaji.
“Yakowapi mashahiri
hayo, ziko wapi nyimbo hizo, ziko wapi ngoma hizo za kusifu bara letu na
kuwakumbusha vijana bara hili liliwahi kutawaliwa,” amesema.
“Ndio maana nimesema
ndani ya CCM hatutakuwa na bajeti ya wasanii tena, hakuna tutabaki na TOT
tutaimarisha chombo chetu kile kama alama na Vijana Jazz basi. Tukienda Arusha
tutawakuta wasanii kule wataimba mashairi, watacheza ngoma.”
Amesema alipopokelewa
makao makuu ya chama hicho aliburudishwa na vikundi vya ngoma, kubainisha kuwa
si kwamba wasanii wa nyimbo alizoziita za kurukaruka ni wabaya, bali kibaya kwa
mtazamo wake ni ujumbe uliomo ndani ya sanaa hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni