DIWANI WA CHADEMA KAKONKO AJIUZULU NA KUJIUNGA CCM.

Medas Amos Mahamile ambaye alikuwa diwani wa kata ya Rugenge wilayani Kakonko kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amejiuzulu udiwani na kukihama chama hicho kwa kile alichodai chama hicho kimekuwa na migogoro ambayo haisaidii jamii katika kuleta maendeleo.
Ndugu Medas amesema anajiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kumuunga mkono rais Magufuli katika juhudi zake ambazo anazifanya katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni