KATIBU WA UVCCM WILAYA YA UBUNGO, LEAH D. MBEKE AENDELEA NA ZIARA YA KIUTENDAJI MATAWINI, KATA YA KWEMBE.
![]() |
| Katibu wa Umoja wa vijana CCM UVCCM Wilaya ya Ubungo Ndg Leah D. Mbeke |
Jana katibu alitembelea matawi 6 na leo ametembelea matawi 3 hivyo bado matawi mawili (2) ambayo yatatembelewa kesho asubuhi saa mbili kabla ya kuanza ziara kata ya Saranga.Katibu amepokelewa na Mwenyekiti wa UVCCM kata ya Kwembe.

Katibu anapita kukagua utendaji wa matawini kuanzia ufanyikaji wa vikao, mikutano ya wanachama wote, mawazo ya miradi, utunzaji wa kumbukumbu n.k
Matawi yaliyoyembelewa ni Msakuzi, King'azi A na King'azi B.
Mpaka Sasa yametembelewa matawi 115 Kati ya matawi 137, Kata 12 Kati ya kata 14 za wilaya ya Ubungo.
Imetolewa na:
TAUSI H. RASHID
KATIBU WA HAMASA
WILAYA YA UBUNGO
DAR ES SALAAM.
#TukutaneKazini


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni