Kangi Lugola: Waliovamia Maeneo ya Jeshi Waondolewe Mara Moja
WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewataka wakuu wa vyombo vya
ulinzi na usalama vilivyopo ndani ya Wizara yake kuwaondoa mara moja
wananchi wote waliovamia katika maeneo ya majeshi nchini.
Lugola
alisema hayo baada ya kulikagua Gereza jipya la Wilaya ya Ruangwa
linalojengwa ambalo lina ekari 100 lakini ekari 20 limevamiwa kwa
kujengwa kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti, ufuta na korosho katika
eneo hilo la Jeshi la Magereza.
Akizungumza
baada ya kulikagua Gereza hilo, mjini Ruangwa leo, Lugola alisema
kuanzia sasa viongozi wa vyombo vyake wahakikishe hawaruhusu mwananchi
yeyote kuingia katika maeneo ya jeshi na atakua mkali kulifuatilia suala
hilo.
Lugola
ambaye pia aliikataa kuipokea taarifa ya ujenzi wa gereza hilo ambayo
ilikua inasomwa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Lindi, Rajabu Nyange,
alisema taarifa hiyo ina upungufu mkubwa na hawezi kuipokea licha ya kua
imeeleza kuhusu ardhi ya jeshi hilo kuvamiwa.
“Mimi
huwa nashangaa sana inakuaje wananchi wanavamia ardhi ya jeshi tena
bila woga, halafu jeshi linakaa kimya linabaki kunung’unika, hii
haijakaa sawa kabisa na kamwe sikubaliani nalo,” alisema Lugola.
Lugola
aliongeza kua, “uvamizi wa ardhi mara nyingi unakua kwa jeshi la polisi
na magereza, mbona Jeshi la Wananchi silisikii hili, kwanini nyie
mnakaa kimya wananchi wakivamia ardhi yenu, sasa nawataka muhakikishe
ardhi ya jeshi popote nchini iliyoporwa inarudishwa ndani ya jeshi, na
wote waliovmia waondooeni haraka iwezekanavyo.”
Kwa
upande wake Mkuu wa Magereza mkoani humo, alisema licha ya ujenzi wa
gereza hilo kuendelea kujengwa lakini ekari 20 ilichukuliwa kimakosa na
kujengwa kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti na ufuta pamoja na
kubangua korosho vinavyomilikiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Ruangwa.
“Jitihada
za ufuatiliaji urejeshaji wa eneo hilo zimefanyika ambapo Mkurugenzi wa
Halmashauri hii ameonyesha nia ya kurejeshwa eneo hlo,” alisema Bakari.
Aliongeza
kuwa, ujenzi wa gereza hilo ambalo linatarajiwa kukamilika Septemba
mwaka huu, unatarajiwa kumaliza msongamano wa wafungwa na mahabusu
kwenye Gereza la Wilaya ya Nachingwea kutokana na mahabusu wengi kutoka
Ruangwa.
Waziri
Lugola alifanya ziara ya dharura katika mikoa hiyo, pia aliambatana na
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu kwa kufanya ziara
ya kutembelea Jengo lililokwama ujenzi la uhamiaji Mkoa wa Mtwara na
Lindi na pia kulitembelea Gereza la mahabusu na wafungwa linalojengwa
mjini Ruangwa, mara baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,
Ulinzi na Usalama kubaini mapungufu ya ujenzi wa majengo hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni