WAZIRI MKUU MGENI RASMI MKUTANO WA MWAKA WA TAASISI YA SEKTA BINAFSI TANZANIA (TPSF)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano wa
14 wa mwaka wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) utakaofanyika
kesho jijini Dar es
Salaam.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey
Simbeye,
maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na utatanguliwa na
mkutano mwingine wa wajumbe kutoka kongani 14 zinazounda sekta binafsi.
"Mkutano
huo ni muhimu sana kwani ndiyo utakaotoa nafasi kufanya uchaguzi wa
wajumbe 14 wa bodi ya wakurugenzi ya TPSF wajumbe hao
ndiyo
watakaopendekeza majina mawili ya wagombea wa nafasi ya mwenyekiti
wa taasisi hiyo," alisema Simbeye.
Simbeye
alieleza kuwa wajumbe 14 kutoka kila kongani watakaochagulia na
kuidhinishwa kwa
kawaida huwa pia ni wajumbe wa Baraza la Taifa la
Biashara (TNBC) wakiungana na wajumbe wengine 14 kutoka sekta ya Umma
ambapo Rais ndiye mwenyekiti wa Baraza.
Alisema
maudhui ya mkutano huo ni ‘Uongozi, biashara unaowajibika katika
ushirikiano wa sekta za umma na binafsi kwa maendeleo endelevu ya
kiuchumi’.
Alisema
wajumbe watakaochaguliwa kwenye mkutano huo watatangazwa na kuridhiwa
na mkutano wa mwaka na kwamba majina mawili yatakayopendekezwa
yatachaguliwa kwenye nafasi za mwenyekiti na makamu mwenyekiti.
"Katika
bodi inayomaliza muda wake, Mwenyekiti alikuwa Dk. Reginald Mengi na
Makamu Mwenyekiti alikuwa Salumu Shamte ambao wamefanya kazi nzuri ya
kuiimarisha sekta binafsi nchini," alisema Simbeye.
Simbeye
aliongeza kuwa mikutano na vikao mbalimbali ambavyo vimefanywa kati ya
sekta za umma na binafsi chini ya bodi inayomaliza muda wake vimekuwa na
mafanikio makubwa.
Pia alisema Novemba 20, mwaka huu TPSF itaadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake.
Aliongeza kuwa TPSF ipo mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za Serikali ya Rais John Magufuli.
“Sisi
sekta binafsi tumejipanga kutokomeza vitendo vya rushwa miongoni mwa
wanachama wetu. Kuimarisha uhusiano wetu na serikali ikiwamo kuhamasisha
ulipaji wa kodi miongoni mwa wanachama wetu pia," alisema Simbeye
Jumuiya
zinazounda TPSF zinajumuisha Kilimo, Viwanda, Utalii, Benki na Fedha,
Madini,Huduma, Wanawake Wajasiriamali, Wafanyabiashara Zanzibar, Ujenzi
na Uhandisi, Mafuta na Gesi, Usafirishaji, Makampuni, Biashara na
Uchuuzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni