Dstv Tanzania

MBUNGE CCM ACHARUKA UBADHIRIFU ULIOFANYIKA JIMBONI KWAKE.

Mbunge wa jimbo la Manonga, Mh. Seif Gulamali ambaye siku za karibuni amegeuka mwiba mkali kwa watendaji wabadhirifu ndani ya wilaya ya Igunga. Wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mh.Kasimu Majaliwa, mbunge huyo aliibua ufisadi wa zaidi milioni 170, na Waziri Mkuu aliagiza wahusika wote kukamatwa.

Leo katika ukurasa wake wa Facebook, Mh. Gulamali ameandika yafuatayo!
______

Katika Kijiji cha Bulangamilwa zimepotea Mil 141 na Mifuko 90 ya saruji,Katika Kijiji hicho hicho cha Bulangamilwa kilipata Mil karibu 700 za Mradi wa Maji Mradi umetekelezwa chini ya kiwango na Maji hayatoki ni Ubadirifu tena wa Fedha za Umma. Siwezi kunyamaza!

Kijiji cha Choma zimetolewa Mil 35 za Mashine ya Mpunga badala yake Mashine ikanunuliwa iliyotumika na mpaka leo hakuna kinachoendelea.Nilipiga sana Kelele juu ya Masuala haya lakini waliweka Nta kwenye Masikio huku wakiendelea kunibeza wakitumia nafasi zao kuwalinda Wezi,Nimeomba kuwatumikia Wana Manonga na wakaniamini kwa Miaka 5 nitahakikisha Fedha zenu za Miradi ndani ya Miaka yangu 5 hazipotei kirahisi tutakula nao Sahani Moja. Narudia tena, haitapotea hata mia moja nikanyamaza!!

Na kwa wale ambao wanawaza kufanya kazi chini ya Viwango ndani ya Jimbo langu hao hawana nafasi na wasipoteze muda wao kwani watarudia kazi zao mpaka wakae sawa.

Kama unawaza kutumia Njia zenu kuja kuniondoa katika Ubunge hilo halinipi shida nitakuwa nimetimiza Kazi yangu niliyoiomba.

UBUNGE sio Ufalme,Udikteta wala Usultani ni UTUMISHI na Niliomba kuwatumikia wana Manonga kwa Miaka 5 na niliwaambia wapiga kura wangu nikishindwa kutimiza Ahadi zangu wanipige Chini kama nitaomba tena.

Niliahidi na Ninatekeleza, Sina Muda wa Kuupoteza

Nipo kazini, Hakuna kulala!!

Hakuna maoni: