Dstv Tanzania

KATIBU UVCCM MKOA-NJOMBE ALIYEWAHI KUTAMBA KATIKA MEDANI YA SOKA NA BADO ANAKIPIGA NA KUHAMASISHA MICHEZO UVCCM.

Na.Titho Stambuli

Katibu asiyebahatisha utendaji wake wa kazi Cde -Sure Mwasanguti, ameonekana kutawala vichwa vya habar hususan katika Mpogoro wa walimu, bodaboda, na kutatua changamoto mbalimbali. 


Hivi karibumi ameonyesha umahiri wa kisoka pale alipoibukia mazoez na kupiga soka la maana na kufunga magoli mawili yasiyo ya kubahatisha katibu huyo fundi anayemudu nafasi ya kiungo mchezeshaji na chenga zenye maudhi kwa mabeki , matukio hayo yaliwastua wengi na kila mmoja kutaman kujua historia yake kisoka .


Kazi ya mtandao huu ni kutaka kukata kiu ya maswali ya wadau wa soka na juu ya historia ya soka ya Comrade Mwasanguti. Akihojiana na stambuli media amewaondoa wasiwasi kuwa amechezea timu mbalimbali mkoan mbeya na mahala pengine ambapo amepita. 


"Mimi mchezo wa mpira nimezaliwa nakipaji sio najifunza leo sijaonekana muda kidogo kwakuwa nimebanwa na majukumu mengi ya kukitumikia chama changu " .


........hayo ndio majibu ambayo tumeyapata lkn bado anadai anataman kulisakata soka pale anapopata muda kwa mazoezi ni muhimu katika maisha yetu huleta mshikamano, umoja, Afya na kukuweka fiti kila muda.

Lakini pia bado ninandoto ya kuhakikisha ndani ya Uvccm soka linakuwepo kwa vijana hususan eneo langu la utawala, uvccm pia inawajibu wa kulea vipaji vya vijana kwani kufanya hivyo ni kutengeneza ajira pia na kuwafanya vijana wawe busy kuhakikisha vipawa vyao haviishii njian. 

Na pia bado amekuwa Mdau na mhamasishaji mkubwa wa michezo kupitia ofisi yake mkoani Njombe,akiamini kwamba ilani ya ccm  bado inaeleza vizur uwajibikaji katika michezo bila kujali lika na kutoa support .

Ninatamani sikumoja kuona UVCCM wanamiliki timu ambayo itakipiga hata ligi kuu na kuliwakilisha taifa kimataifa, yote haya inawezekana endapo tutadumisha mshikamano katika swala zima la michezo.........

Ni hayo tuu ambayo tumekuletea kutoka kwa kiungo mchezeshaji Comrade Mwasanguti

Hakuna maoni: