KATIBU WA UVCCM WILAYA YA UBUNGO, LEAH D. MBEKE AENDELEA NA ZIARA YA KIUTENDAJI MATAWINI, KATA YA SARANGA.
![]() |
Katibu wa Umoja wa vijana CCM Wilaya ya Ubungo Leah D. Mbeke |
Katibu amepokelewa na katibu wa CCM kata ya Saranga, ndugu: Romanus Songambele, Katibu wa Uvccm kata ndugu: Enock Haule na mjumbe wa kamati ya utekelezaji kata ndugu: Frank Michael.

Katibu anapita kukagua utendaji wa matawini kuanzia ufanyikaji wa vikao, mikutano ya wanachama wote, mawazo ya miradi, utunzaji wa kumbukumbu n.k
" kata ya Saranga naidai vijana 1500 sababu mna matawi 15, nimeagiza mikutano ya wanachama wote vijana, waje muwasikilize na myafanyie kazi watakayoyasema, kila Tawi lifanye mkutano wake na muhstasari niletewe na niwahakikishie nitaipitia yote kuisoma!." alisema katibu Leah.

"Kuna tabia viongozi wa kiserikali wakishika nafasi tu wanakuwa marafiki wa viongozi wa Chama na wanaitenga jumuiya ya vijana, vijana wakiwahitaji mpaka Chama kiseme nenda ndio aende kushiriki na vijana, hili halikubaliki! Vijana wapewe heshima yao...kiongozi wa kiserikali ni wa wote na dhamana ya kulinda serikali ni ya vijana hivyo msiwawekee vijana mipaka ya kuwasiliana na kiongozi wao!!" alimalizia katibu huyo kwa msisitizo.
Matawi yaliyotembelewa siku ya leo ni Matangini, Kimara B, Mji Mpya, Busara, Michungwani, Amani na Hekima.
Mpaka Sasa yametembelewa matawi 124 Kati ya matawi 137, Kata 13 Kati ya kata 14 za wilaya ya Ubungo.
# Ziara hii inaendelea kata Saranga inaendelea kesho.
Imetolewa na:
TAUSI H. RASHID
KATIBU WA HAMASA
WILAYA YA UBUNGO
DAR ES SALAAM.
#TukutaneKazini
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni