KATIBU HAMASA NA CHIPUKIZI WILAYA YA NJOMBE ATOA SEMINA YA UONGOZI KWA VIONGOZ WA KATA NA MATAWI UVCCM NJOMBE.
![]() |
Katibu wa Hamasa na Chipukizi Wilaya ya Njombe Iman Mahmoud Moyo |
Na.Titho Stambuli.
Ndugu Iman Mahmoud moyo amezidi kuimarisha idara yake ya hamasa na chipukizi wilaya ya Njombe kwa kutoa semina elekezi ya uongozi kwa watendaji na viongoz ngazi za kata na matawi ili kuhakikisha viongoz hao wanakuwa wazalendo kwa chama chao na utendaji uliotukuka.
Semina hiyo imefanyika Leo 18/08/2018,katika ukumbi wa CCM wilaya ya Njombe.
Cde moyo anayebamba katika medani ya siasa kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kunukuu kumbukumbu za Baba wa taifa Mwalimu Julius kamabarage Nyerere ametoa semina ya uongozi na utawala, kuibua miradi ndani ya Kata na Matawi, mahusiano na maadili ya kiuongozi .
Semina hIyo imefana kwa kuwa kila alichokifundisha kimeonekana kuwagusa walengwa na kufurahia kupata elimu hyo ambayo imewajengea uwezo mkubwa katika kukitumikia chama cha mapinduzi na kuwa wazalendo.
Akitoa mafunzo ya semina hyo amewataka kulinda maadili ya kiungozi na kuwatumikia wananchi na kuisadia Serikali kubaini changamoto zinazowasumbua wananchi ziweze kutatulia, kwasababu Mmepewa dhamana ya kuwaongoza watu ni Lazima tuwatumikie watu wetu.
Pia ameweza kuwakumbusha ni vigumu kuongoza watu bila kuwasaidia wawe na uchumi wa kujitegemea hakuna tutakacho kuwa Tumefanya ni lazima tuwe wakombozi wa kiuchumi na ndio ukombozi tunaoutafuta Kwa sasa kwa kuwa uhuru tulishaupata.
"ili uwe kiongozi bora ni lazima ufanye kazi uwe na uchumi hata jamii unayoiongoza inakuwa na imani nawewe, tutumie fursa zinazotuzunguka ili kuweza kujikomboa kiuchumi "
Moyo ameweza kuzungumza na mtandao kuwa hii semina haiwez kuwa ndo mwisho kila mara tutazd kuwakumbusha viongoz hawa namna gani wawatumikie na amefurahi kuona mwitikio wake kwa viongoz hawa na inampa matumaini ya kuzidi kusonga mbele na viongoz hawa katika kukilinda chama cha mapinduzi na uzalendo kwa taifa letu.
Lakini pia amewataka kutokuwa wanyonge pale wapinzani wanapokuwa wanaharibu Hali ya hewa nchi imetulia mheshimiwa raisi, wabunge, madiwani na wenyeviti wanapga kazi mwingine kazi yake ni kuharibu hii haikubariki ni lazima tupambane na watu wa aina hii vijana wa ccm hatuwezi kukaa kimya.
"tumepewa dhamana kuongoza Serikali ni lazima tutumie gharama kuilinda na ila hatukatazwi kuikosoa Serikali Kama inayumba nao ni wajibu wetu kama vijana hapo hatupaswi kuwa waoga kwa maslahi ya taifa letu"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni