KATIBU UVCCM W-LUDEWA ATEMBELEA KITUO CHA AFYA LUILO KUKAGUA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM
Na.Titho Stambuli
Katibu wa uvccm Cde -Hassan Kapolo ambaye ndiye Mtendaji mkuu ngazi ya vijana wilaya ya Ludewa ameweza kufika katika kituo cha Afya luilo kujionea ujenzi wa kituo cha Afya kinachojengwa kwa Nguvu za wananchi na Serikali imechangia shillingi million tano.
Yeye ndiye mwenye chama kinachoongoza Serikali ameona umuhimu wa kukagua kituo hicho kwakua ndio wajibu wake kuona shughuli zinavyokwenda kwakuwa ndiye mkaguzi wa ilani ya CCM na Serikali ndiyo watekelezaji.
"nimefika kata ya luilo kuona ujenzi wa kituo hiki kwakuwa CCM tuliahidi kufanya kazi na kusogeza huduma karibu kwa wananchi "
Akizungumza na mtandao huu amesema anatamani huduma ziwaishwe ili kazi ziendelee, huduma kwa wananchi kwakuwa ndio mkataba wetu na wananchi.
Aidha amempongeza mh DC Andrea Tsere kwakuwa amekuwa bega kwa bega kuhakikisha ila ya CCM inatekelezwa kwa kushirikiana na wananchi ,sisi kama jumuiya ya vijana tunaridhishwa na utendaji huu wa kazi na tunaomba wananchi waendelee kuunga mkono juhudi za Serikali.
Lakini pia waendelee kukiamn chama cha mapinduzi kwa kuwa tunatekeleza ahadi zetu zote tulizo ahidi.
Sisi Stambuli media tunakutakia kazi njema
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni