KATIBU WA UVCCM WILAYA YA UBUNGO, LEAH D. MBEKE LEO AMEHITIMISHA ZIARA YA KIUTENDAJI MATAWI 137 YA WILAYA YA UBUNGO.
Leo tarehe 21/08/2018 katibu wa Umoja wa vijana CCM , ndugu: Leah D. Mbeke pamoja na mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM wilaya ndugu: Yusuph Ramadhan, wamehitimisha ziara ya kiutendaji matawini kwa kutembelea matawi tisa (9) ya kata ya KIMARA iliyokuwa kata ya mwisho katika kata 14 za wilaya ya Ubungo.
Katibu amepokelewa na mwenyekiti wa UVCCM kata ndugu: Clieff Mtapai Katibu wa CCM kata ndugu: James Kalabaka.
Katibu katika ziara hi amepita kukagua utendaji wa matawini kuanzia ufanyikaji wa vikao, mikutano ya wanachama wote, mawazo ya miradi, utunzaji wa kumbukumbu n.k
" Kwanza kabisa ninamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kumaliza ziara hii, nakiri haikuwa kazi rahisi..lakini kwa ajili ya upendo wa kusaidia vijana nimekamilisha na nimejua vitu vingi Sana, lakini pia nawashukuru wajumbe wa kamati ya utekelezaji kwa ushirikiano, viongozi wote wa kata 14 na wa matawi yote 137 na mawili yanasubiri kuzinduliwa tu, ahsanteni sana sana." alisema katibu Leah.
"Niwaombe kushikamana kwelikweli na tusaidiane, hi jumuiya ni yetu sote ." alisisitiza katibu huyo
"Nimezunguka matawi yote 137 ya wilaya nzima ya Ubungo na mengine mawili yanayoenda kuzinduliwa hivyo matawi 140 nimepita na kutengeneza jumuiya kwa kutoa maagizo mbalimbali..Sasa ni ufatiliaji wa utekelezaji wake hapo ndipo tutajua ni yupi anatuulia jumuiya." alimalizia katibu huyo kwa msisitizo.
Matawi yaliyotembelewa siku ya leo ni Kwa Mtoro, 770, Baruti, Nzasa, Kilungule Tanesco, Kilungule A, Matete, Mavurunza na Milenia ya tatu.
Imetolewa na:
TAUSI H. RASHID
KATIBU WA HAMASA
WILAYA YA UBUNGO
DAR ES SALAAM.
#TukutaneKazini

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni